Maji Ya Moto Hayaunguzi Nyumba

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maji ya moto katika usemi huu, tunamaanisha maneno maneno hayavunji mfupa. Ni kawaida kabisa kila siku iendayo kwa Mungu sisi binadamu, muda mwingi tunautumia kwa kusemana semana na kufanyiana vurugu nyingi za hapa na pale. Hata pale inapoonekana kuwa mtu anajihangaisha bila kuchoka ili kujitafutia riziki yake, vimaneno maneno huwa ni vingi sana.  

Haya yote hufanywa ili kumkatisha tamaa mhusika. Maneno yanayosemwa dhidi yako, mara nyingi huwa ni ya maudhi kiasi kwamba   yanaweza kukukatisha tamaa kabisa. Unaweza hata ukaacha kuendelea kuhangaika na shughuli zako za kimaendeleo.

Ushauri wangu ni kwamba, unatakiwa kuyapuuza maneno hayo kwa sababu hayakupunguzii chochote katika maisha yako. Kama ule usemi wa “Watasema mchana, usiku watalala”, kwenye hali hii, msemo huo una maana sana. Wewe kwa upande mwingine, utakuwa ukiendelea na shughuli zako kama kawaida. Wao wataendelea kubwabwaja wee mpaka wachoke.

Ndio maana ya usemi huu wa maji ya moto, pamoja na ukali wake hayawezi kuunguza nyumba. Hata watu waseme namna gani wewe utabaki vile ulivyo, sana sana wao ndio watapata taabu wakikuona kuwa hutetereki hata kidogo. Cha msingi, wewe endelea kujiamini na kutekeleza yale uliyoyapanga.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: