Acha Kuishi Kwa Wasiwasi, Hapo Ulipo Bado Una Nafasi

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maisha ni kupanda na kushuka. Chochote utakachokifanya, ni lazima utapitia changamoto za aina mbali mbali. Changamoto hizo zisikufanye uishi kwa wasiwasi na pia zisikukatishe tamaa.  

Unapopambana ná changamoto katika jambo moja, jaribu kuangalia kama kuna jambo jingine ambalo unaweza kulifanya kwa urahisi zaidi. Cha msingi, inakupasa usonge mbele. Jambo moja gumu lisikukatishe tamaa ya kufanya jambo jingine ili uweze kusonga mbele. 

Hata hivyo, kabla ya kuanza jambo jingine, inabidi uangalie kwa makini ili kuona kama hilo jambo linaweza kufanyika. Kufanya hivyo ni muhimu ili kuweza kuzijua mapema changamoto unazoweza kukutana nazo ili uweze kujiandaa mapema namna utakavyoweza kuziepuka ama kuzitatua. 

Yakupasa uondoe wasiwasi. Bado una muda mwingi wa kuweza kufanya mambo mengi. Inawezekana pengine hilo jambo lililokushinda, siyo moja ya yale ambayo umepangiwa kuyafanya na kufanikiwa. Unaposhindwa hili, jaribu lile, pengine hilo unalolijaribu ndilo litakalokupeleka kwenye ushindi. Mambo mengi huja kwa mpango. Yatupasa tukumbuke pia kuwa mambo mazuri hayataki haraka. Mambo mazuri yatakiwa kufanyika kwa subira ili yatoe matunda mazuri.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: