Mtandao Ni Uwanja Wa Ulaghai

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Baadhi ya wasichana wamekuwa wakirubuniwa na baadhi ya wanaume wanaoishi nchi za nje. Warubuni na warubuniwa, hukutana kwenye mitandao ya kijamii. Utandawazi ndio chanzo kikubwa cha kuleta yote haya. Mahusiano huanzia hapo, kwenye mitandao, juu kwa juu. 

Kwani inakuwaje? Mwanamme humdanganya msichana na kumshawishi kuwa akienda ughaibuni, atamuoa. Mabinti wa siku hizi ni wa ajabu sana. Anaamini hadithi hiyo ya kuolewa juu kwa juu. Huyo bwana maskini hata hamjui🤷🏽‍♂️. Hana taarifa zozote zinazomhusu huyo mwanamme.

Kuna kisa cha  msichana mmoja aliyekuwa na kazi yake nzuri tu serikalini. Alikuwa amepewa na usafiri wa kazini. Pia alikuwa ameanza kujenga nyumba yake ya kuishi. Lakini kwa kudanganywa na mwanaume asiyemjua, aliyekuwa akiishi huko nje ya nchi, alijiharibia maisha yake. 

Binti bila kufikiria kwa kina, aliacha kazi ndani ya masaa 24. Aliuza vitu vyake vyote na vingine akavigawa. Tileti ya ndege ilitumwa haraka haraka, na binti akaona, “mambo si hayo”. 

Baada ya kukamilisha mambo yake, binti alifunga safari yake na kumfuata huyo mwanaume asiyemjua huko aliko! Ni ajabu na kweli. Alipofika, alipokelewa vizuri. Mwanaume alionyesha mapenzi ya kweli kweli mpaka msichana akaona maisha ndio hayo. 

Kumbe lakini mwanaume huyo wala hakuwa na mpango wa kumuoa huyo msichana. Kama ilivyo desturi ya wanaume wengi, yule mwanaume alitaka amtumie tu na si vinginevyo.

Wawili hawa waliishi vizuri kwa mwaka mmoja. Huyo mwanaume alimtafutia kazi. Alikuwa anaenda kumchukua kila siku baada ya kazi ili kumwonyesha kuwa anampenda kwa dhati. Waliendelea kuishi kwa raha bila ugomvi wowote kwa mwaka mmoja.

Baada ya mwaka moja, yule kijana alimwambia msichana arudi Tanzania kuwasalimia wazazi. Alidai kuwa yeye ana kawaida ya kwenda Tanzania kila baada ya miaka minne, kwa hiyo muda wake ulikuwa bado haujafika. 

Msichana alikataa kwenda kuwaona wazee wake lakini kijana alichukua muda kumbembeleza. Alimfanyia shopping ya nguvu kwa ajili ya wazazi na ndugu wengine. Hatimaye, msichana alikubali

kurudi Tanzania na baada ya wiki akataka kurudi tena alikotoka, kwa yule kijana. Lakini kijana aliongea naye na kumwambia akae kwa mwezi moja na ndipo atamtumia tiketi. Msichana aliamini maneno hayo. Lakini baada ya hapo kijana akawa hapatikani tena , si kwa simu wala barua pepe.

Jinsi muda ulivyozidi kupita, mambo yalibadilika. Hatimaye, ukweli ulijitokeza. Alitokea kijana mmoja aliyekuwa anamfahamu yule jamaa mlaghai. Bila kumung’unya maneno, alimwambia msichana kuwa yanayompata huyo binti, yaliishampata msichana mwingine tena. Aliendelea kumtonya kuwa msichana huyo alikuwa mwalimu. Bila kumficha, alimwambia kuwa mwalimu huyo alifanyiwa hivyo hivyo na huyo kaka. Hivyo yanayompata huyu dada siyo mageni maskioni mwa watu. Binti huyo alitumiwa na huyo kijana kwa miaka miwili. Baada ya hapo, mwalimu alikuja kuachwa solemba. 

Hapo ilijulikana kuwa huo ndio ulikuwa mchezo wa huyo jamaa. 

Wako wengi wenye tabia za namna hii. Wasichana wengi, hasa wale wapenda maisha ya mteremko wamekuwa wakiingia mkenge mara nyingi tu kwa watu wa aina kama ya kijana huyu.

Yapo mengi ya kujifunza kutoka kisa hiki, hususani, kwa vijana. Baadhi ya mafunzo hayo ni haya yafuatayo:

1. Vijana wanaaswa kuwa makini katika kuingia kwenye mahusiano. Haiingii akilini kijana anamfuata mtu asiyemjua huko ughaibuni. Mahusiano ni lazima yaambatame na upendo, na si vinginevyo!

2. Vijana, wajifunze ubaya wa mitandaoni. Wanaonyeshwa ubaya wa kujihusisha na mapenzi ya mtandaoni kuwa siyo halisia. Siyo rahisi kumjua mtu kwa undani kupitia mtandao. Hapa nchini tuna taratibu zetu za kuoa ama kuolewa. Familia zote mbili, za muoaji na muolewaji huwa zina utaratibu wa kuchunguzana kwanza kabla hawajaridhia muunganiko wa hao wawili (watoto wao) ufanyike. Mahusiano ya kwenye mtandao hayatoi fursa kwa huu mchujo kufanyika. 

3. Vijana jifunzeni kuwa maisha ni popote, siyo lazima kwenda nje ya Tanzania. Acheni ulimbukeni wa kufikiria kuwa ughaibuni ndiyo kuzuri zaidi na kuna fursa nyingi. Tulizaneni hapa hapa nchini ili muweze kuishi maisha mazuri na yenye usalama zaidi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: