
Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Kazi ndio msingi wa maisha. Binadamu sote hujishughulisha na kazi ili waweze kuishi. Katika mchakato huo wa kufanya kazi, unakutana na watu wengi ambao nyote mpo kwa ajili ya kufanya kazi na kupata riziki.
Mara nyingi sehemu nyingi za kazi huwa zina changamoto zake ambazo husababishwa na wafanyakazi wenyewe. Karibu mara zote, chuki huelekezwa kwa mtu ambaye ni mfanyaji kazi mzuri. Watu humuonea wivu. Watu hufikia hatua ya kwenda kumfitinisha mfanyakazi huyo kwa bosi. Hupeleka maneno ya uchonganishi. Katika fitina hizo, wafitini hao hujitahidi kumrubuni bosi kwa maneno yatakayoonyesha kuwa wao ndio wafanyakazi
bora kuliko huyo anayesifiwa na kila mtu. Hali kadhalika, watamshawishi bosi aone wao ndio wafanyakazi wazuri. Bosi asipokuwa makini, anaweza kuyumbishwa.
Simulizi hii ilimpata msimulizi mwenyewe kwenye Wizara aliyokuwa anafanya kazi. Ilitokea kwamba msimulia kisa hiki alikuwa amepata bahati ya kuchaguliwa kuongoza kitengo fulani hapo hapo Wizarani. Kumbe watu hawakuridhika na uchaguzi huo. Vita kubwa ilianza kutoka kwa watumishi wenzie. ilikuwa sio ya kawaida. Wafanyakazi wenzie walionyesha wazi kumchukia bayana mteuliwa huyu. Kwa kweli kulikuwa na hali ya chuki ya waziwazi kutoka kwa mahasidi ambao walikuwa hawakupendezwa na uteuzi wa mwenzao. Kulitokea ‘tension’ kubwa sana.
Ilifika siku moja bosi alishindwa kuvumilia utesi huu dhidi ya yule mteule wake. Aliona kuwa hakukuwa na sababu zozote za msingi. Aliamua kuwatolea uvivu watesi hao na kuwaeleza ukweli. Aliwaambia kuwa wasione ajabu kuwa amemuweka mwenzao kuwa Mkuu hapo idarani. Aliendelea kwa kusema kuwa utendaji wake wa kazi ndio umemuweka hapo, na si vinginevyo. Aliwaambia hata ninyi mkitaka kuwa kama yeye, itawapasa mfanye kazi kwa bidii, la sivyo wataishia kulalama tu bila mafanikio.
Tamko la Mkuu wa kazi lilisaidia sana kuweka sawa hali ya hewa pale idarani. Baada ya hapo watesi walilazimika kubadilika na kuwa karibu na mwenzao waliyekuwa wakimsema. Walitaka wajifunze kutoka kwake ili nao waweze kufanikiwa siku moja.
Jamani, hata maandiko matakatifu yanasema:”Asiyefanya kazi na asile”. Kila mtu yampasa ajitahidi kufanya kazi kwa kadri ya uwezo wake, kwenye nafasi yake aliyo nayo. Si rahisi kupanda ngazi kwa kumchafua mwenzio. Cha msingi, ni lazima ujue kuwa utatambulika kutokana na utendaji wako wa kazi na si vinginevyo. Waswahili husema, “Mtaka cha Uvunguni, Sharti Ainame”. Mwenzao aliinama kisawasawa, kazi yake ikaonekana na kutambulika kwa Wakuu. Ukweli ni kwamba, kila mtu atapata kile anachostahili.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection
Fab
I’m so glad to find a site like this. This is very helpful.
Jess
http://befitandhealthy.net/
LikeLiked by 1 person
Thank you Jess! We are happy you are here.
LikeLike