Kaa Mbali Na Mazoea

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Mazoea ni ile hali ya kulizoea jambo au kumzoea mtu. Katika kumzoea mtu inafikia mahali mtu anajisahau na kujikuta anasimulia mambo yake yote. Kwa kufanya hivyo, anafikiri ni sifa. Hajui kama anajianika na kujidhalilisha kwa kueleza mambo yake kwa watu. Ukweli ni kwamba, hakuna siri ya watu wawili. Kuna mazoea mengine ya kwenye sehemu za kazi ambayo nayo pia huwa ni ya hatari. 

Kulikuwepo kijana mmoja alitumia muda mrefu sana kutafuta kazi. Hatimaye, Mungu alimjalia, akaja akapata kazi kupitia rafiki yake ambaye alikuwa ndio boss wa hiyo kampuni. Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana. Ghafla alisahau tabu zote alizopata kutafuta kazi. Badala ya kuiheshimu kazi, alikuwa akifanya vile anavyotaka, eti kwa sababu boss ni rafiki yake. Alikuwa na jeuri kwa wenzie hapo kazini. Alifanya kazi kwa mazoea akiringia urafiki wake na boss. Mara nyingi alikuwa anachelewa kufika kazini kwa sababu tu ana urafiki na boss. 

Haukupita muda, boss akahamishwa. Katika hali ya kawaida yule kijana angebadilika kufuatia uongozi kubadilika. Lakini yeye, kwa akili yake finyu, alidhani na yule boss mpya atakuwa anambeba kama yule wa zamani. Maskini, mambo hayakuwa hivyo. Boss mpya hakusherehekea uzembe katika kazi. Jamaa alianza kuandikiwa barua za maonyo mara kwa mara. Tabia yake haikuweza kuvumilika. Mwishowe ilibidi yule jamaa afuluzwe kazi. Kwa kweli, alistahili adhabu hiyo. 

Ni mara ngapi watu tunapenda kuizoea mamlaka iliyo juu yetu? Anayekuongoza hatakiwi kuzoeleka sana. Kwa vile umemzoea sana unaweza ukajikuta unamkosea na unaweza usitambue hilo, ya kwamba umemkosea. Wewe utakuwa unaona kuwa mko sawa tu. 

Yatupasa tuheshimu mamlaka yoyote iliyopo juu yetu. Hata kama mamlaka zilizopo mnaweza kuwa mnalingana kielimu ama kiumri, ili mradi tu wana mamlaka, yatupasa tuweke hayo yote pembeni ili tuweze kutenda haki na kutimiza wajibu. 

 Ni lazima tuheshimu na kutekeleza yale tunayoambiwa kwa kadri ya maelekezo yaliyotolewa. Tufike mahali tuondoe mazoea bali tuheshimu mamlaka.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: