Fikra Zako Usimshirikishe Mtu

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maisha yetu katika ulimwengu huu ni ya vurugu kati ya mtu na mtu. Chochote mtu akifanyacho kimeanzia kwenye fikra zake. Kwa kawaida, mtu hawezi kukurupuka tu na kuanzisha kitu bila kufikiria na kupembua kama hilo jambo litawezekana ama la. Mara nyingi, tunafanya kosa kumshirikisha mtu ama watu mawazo yetu mapema mno. Inawezekana, huyo unayemshirikisha hawezi kukutia moyo ili ufanikiwe, binadamu wengi ndivyo walivyo. Wengi hupenda kukatisha tamaa wenzao na hata kunena maneno mengi ambayo yanaweza kukutoa kwenye wazo lako. 

Cha kushangaza lakini, mwisho wa siku unaweza kuja kuona kuwa yeye uliyemshirikisha na akakukatisha tamaa ndiye anayelitumia wazo lako lilelile kulitendea kazi. Utabaki unashangaa unapoona mawazo yako uliyomshirikisha ndio yanayomnufaisha sasa. 

Nina hakika hata mkurugenzi wa TEWWY alipopata wazo la kuanzisha shirika la TEWWY wapo ambao walijaribu kumkatisha tamaa kuwa hataweza, lakini naona alikomaa ndio maana tupo hapa mpaka leo. 

Hebu tuangalie tulikotoka wana TEWWY. Ni wangapi tulikuwa nao mwanzoni, lakini leo hatunao, waliondoka kwani waliona hiki kitu hakina maana kwao. Lakini leo hii, katika kundi la ngo’s, na sisi TEWWY tupo, tunaifanya kazi ya Mungu ambaye anauona umuhimu wetu kwenye jamii. 

Mambo mazuri hayataki haraka tutafika mahali tutasimulia matendo makuu huko baadaye. Tuna shuhuda nyingi tu za kusimulia zinazohusu watu walionufaika na huduma zetu za unasihi. 

Ni fundisho kwa kila mwanadamu kutoshirikisha wazo lake kabla halijawa tayari ili kukwepa yanayoweza kutokea, aidha kunyang’anywa wazo lake juu kwa juu, ama kukatishwa tamaa ili asiendelee na wazo lake. Mara nyingi, binadamu siyo wema, hupenda kuharibu mipango ya wenzao kwa makusudi. Ni vema kushirikisha mtu wazo lako ukishaona limeiva, liko tayari kwa utekelezaji.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: