Kuna Wakati Wa Kuwaacha Au Kuwapoteza Uliowazoea

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Hofu kubwa ambayo kila mtu anayo kwenye maisha ni kupoteza au kuwa mbali na watu tuliowazoea. Hata hivyo, katika safari yako hapa duniani, kuna wakati utalazimika kukubali kupoteza baadhi ya watu. Siyo lazima hali hiyo isababishwe na chuki au ugomvi, bali kuna wakati inabidi iwe hivyo.

Kuna watu wanaweza kuambatana na wewe, ili mradi tu uko chini yao. Ukianza tu kuinuka kidogo, wao hulazimika kukaa mbali na wewe, la sivyo watageuka kuwa mwiba kwako. Kuna watu ambao wakiendelea kuwa karibu sana nawe wanaanza kutumia nafasi yao ya kukujua wewe. Watu hawa hutumia madhaifu yako kama silaha ya kukuangusha. Wapo wengi hao, yatupasa tuwe waangalifu. 

Kuna watu ambao unapoanza kujiamini na kupambania ndoto yako kubwa, hukugeuka na kuwa adui zako. Kwa watu wa namna hii, wangependa uendelee kuwa mtu wa kawaida, mtu wa chini. Ukiwa hivyo, hawatakuwa na shida kabisa na wewe, hautakuwa tishio kwao. Chuki inaanza pale utakapoanza tu kupambania ndoto zako kubwa, kamwe hawatapenda upande.

Wako tayari wakae na wewe na wakusaidie, endapo tu utakubali na kuridhia matakwa yao ya wewe kuendelea kuwa mdogo, usiwe na maendeleo. Kupanda kwako ni homa kubwa sana kwao, ukianza kujaribu kuwa mkubwa tu, wanakugeuza adui.

Mahusiano ya namna hiyo ni mahusiano yenye sumu. Ni mahusiano ambayo yanachosha. Muda ukifika wa kuachana na watu wa namna hiyo, fanya hivyo haraka, lakini kumbuka, sio lazima iwe kwa ugomvi. Inakupasa uachane nao kwa amani, bila mtafaruku wowote. Unapopambana na haya, usiogope kwani hiyo ni sehemu mojawapo muhimu ya kukua kwako. Yatupasa tujifunze, ni wajibu wa kila mtu. Maisha ndivyo yalivyo, ni kujifunza kila uchao. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: