Kosa Moja Halimuachi Mke

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kosa ni kufanya jambo ambalo sio sahihi au liko nje ya makubaliano au kutenda jambo kinyume na jinsi inavyotakiwa. Katika maisha ya binadamu mke na mume wanaweza kutendeana makosa wao kwa wao. Mwanamke hutumia muda mwingi kukaa nyumbani na ndiye anaetunza familia na kuyabeba majukumu  mbalimbali ya familia.

Hivyo, akikosea hapaswi kufukuzwa kwani kosa linaweza kusuluhishwa kwa njia ya kuongea na pia kusameheana. Kukoseana kupo wakati wote. Ndugu, jamaa na marafiki huweza kukoseana mara kwa mara, hivyo ni jambo la kawaida, siyo la ajabu. Lakini, kama binadamu, inatupasa tujitahidi kutowakosea binadamu wenzetu, hususani, ndugu, jamaa na marafiki na watu wote wanaotupenda. 

Pale tunapokoseana, ni vema tukawa na maridhiano ya kusameheana ili tuishi kwa amani, upendo na furaha. Wahenga hunena, kutenda kosa si kosa, bali kurudia kosa. Kila mkosaji anapaswa kuomba msamaha, ndio ubinadamu, ndio utu. Ni utaratibu na uungwana pia kuwa kila aombaye msamaha apewe. Huo ndio ubinadamu na hivyo ndivyo tunavyotakiwa kuishi. Binadamu ni viumbe wenye akili na utashi, tumeumbwa tofauti na wanyama. Yatupasa tuishi vile tunavyotakiwa kuishi na hapo tutapata baraka kutoka kwa Muumba wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: