
Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Hapa duniani siyo rahisi kuwafanya watu wote wakupende hata kama unafanya mema. Si ajabu ukaona kuwa yule uliyemfanyia mema ndio atakayeanzisha ligi ya kukuchukia na hata kuwafanya wengine wakuchukie. Kama Muumba wetu huwa tunamchukiza kila iitwapo leo na bado anatupa uhai na riziki sembuse sisi binadamu? Kutendeana maovu wenyewe kwa wenyewe na hata kuumizana, si jambo geni na si ajabu kabisa. Inatokea kila siku.
Tofauti iliyopo kati ya Muumba na sisi binadamu ni kwamba chuki za binadamu hazina tija, hazina kichwa wala miguu. Chuki zetu zinaweza zikatupelekea hata kudhuriana na kuumizana. Hatuachi kulalamika na kuona kuwa hatuna bahati na watu. Tunasahau kuwa Yule Aliye juu anatupenda pasipo ukomo na ndio maana tunaishi.
Kwa kawaida, binadamu anapochukiwa, anapata njia ya kutengeneza mapito yake ya kumuongoza kwenye maisha yake ya hapa duniani
Kuna faida ya kuwa na maadui kwenye maisha. Moja ya faida kubwa ni kupunguza idadi ya watu wanaokutegemea. Usilalamike wala kusikitika unapojikuta umetengwa na watu. Hapo unakuwa unatengenezewa kesho yako iliyo nzuri. Wakati ukiwa umetengwa, utashangaa kwani kutoka kusikojulikana, atainuka mtu wa kukusaidia, mtu ambaye hukumtegemea kabisa.
Tunaaswa kuwa tusiishi kwa kumtegemea fulani. Yatupasa tuwe na subira kwani mtu wetu, yu njiani, anakuja. Mungu amemfanyia kila mtu kitu chake, kitu ambacho mwingine hana. Hivyo ndivyo Mungu alivyotuumba, kila kiumbe na riziki yake.
Kuchukiwa ni sehemu ya maisha, hivyo hatuna budi kukubali. Kumbuka, siyo lazima ukukubalike na kila mtu hapa duniani. Kutofautiana ni kawaida kabisa.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection