Changamoto Zako Zisikufanye Uwe Mbishi

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Ukiwa kwenye shida usisahau shida za wengine. Kuna nyakati ambazo njia ya kukutoa kwenye shida zako imefichwa kwenye namna unavyowasaidia wengine wenye shida. Ukiwa kwenye shida , usiwasahau wanaokutegemea. Njia za Mungu hazichunguziki. Hata vitabu vitakatifu vinasema, ni bora kutoa kuliko kupokea.

Jifunze kutoa hata kama na wewe una shida zimekuzonga. Ukubwa wa shida unatofautiana. Pengine shida yako ni ndogo sana ukilinganisha na ya yule. Kusaidiana ni wajibu wetu, wajibu wa kila mwanadamu.

Usiwadharau watu. Usimpime mtu kwa muonekano wake. Usimhukumu mtu kabla ya kumfahamu vizuri, na hata ukimfahamu vizuri, kazi ya kuhukumu siyo kazi yako. Huna haki ya kusema, huyu atanisaidia nini. Huwezi kujua baraka zako utazipata kwa njia gani au kupitia kwa nani. 

Ni kawaida sana kuona watu wakiwa kwenye shida wakitaka wao tu ndio wahurumiwe na wasaidiwe. Huu ni ubinadamu, mara nyingi ni vigumu kuuacha. Lakini inatubidi tuuache, kwani ni tabia ambayo haipendezi. Hali kadhalika, wengi  hatujui kuwa hata ukiwa kwenye shida bado unaweza kuonyesha huruma na upendo kwa wengine. Wengi wamepishana na miujiza yao kwa sababu wakiwa kwenye shida wanajiwazia wao tu na kusahau kabisa wajibu wao kwa wengine. 

Kupitia mazungumzo haya, yatupasa tujifunze kuwa tunapokuwa kwenye changamoto na shida mbali mbali tusisahau wajibu wetu wa kusaidia na wengine. Wako walio na changamoto nzito kuliko zetu, hivyo tunaaswa tusiweke uzito kwenye matatizo yetu peke yake, tuyaangalie na yale ya wenzetu, tutabarikiwa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: