Marafiki Wengi Huongeza Maadui

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Marafiki ni wazuri sana, na pia wanaweza kuwa wabaya sana. Mara nyingi marafiki wale wabaya huja kwako wakiwa kwenye shida. Ajenda ya hawa huwa ni moja tu. Hutaka kusaidiwa na wewe kwenye mambo yao waliyokwama, baada ya hapo huwa ni kwa heri.

Utamjuaje rafiki wa kweli? 

Ni rahisi. Rafiki wa kweli utamjua wakati una shida. Rafiki wa kweli ni yule ambaye atakutia moyo katika mapito yako. Rafiki wa kweli atakuwa nawe katika kipindi chote cha shida. Atakuhifadhia mapito yako na siri zako, hatatangaza kwa watu. Yeye huona kuwa jambo lako ni sawa kabisa na jambo lake. Rafiki wa kweli huweka marafiki zake kwenye sehemu muhimu ndani ya moyo wake. 

Utamjuaje rafiki wa uongo ama rafiki mbaya? 

Ni rahisi pia. Ukweli ni kwamba, mara nyingi anayegeuka kuwa adui mkubwa ni yule uliyekuwa unakula na kunywa nae. Madhaifu yako yote atakuwa anayajua. Kwa vile anajua mapungufu yako, anaweza akayaanika hadharani ili mradi tu akufanye uonekane huna maana mbele za walimwengu. Rafiki mbaya hufurahia kuyaanika mabaya ya wenzake. Daima yeye hutaka kuonekana kuwa ni mjuaji ambaye anazibeba siri nyingi za watu. Kwake yeye, hiyo huwa ni sifa kubwa.

Yatupasa tufanye nini basi? 

Ni lazima tuhakikishe tunakaa mbali na watu wasiokuwa na faida kwetu. Pale unapoona huna cha kupoteza kwa kukaa mbali na mtu fulani, basi fanya hivyo. Huna sababu ya kubeba mizigo isiyobebeka, epuka kujipa tabu zisizo na tija. Ukiwa naye na usipokuwa naye hupotezi chochote katika maisha yako. Kwa nini uhangaike? Yakupasa utafakari sana katika kuchagua marafiki.

Mara nyingi, urafiki ukivunjika, uadui huzaliwa. Uadui unaotokana na kuvunjika kwa urafiki huwa ni mzito na mgumu sana. Kila mmoja huvutia upande wake ili yeye aonekane kuwa ni mzuri kuliko mwenzie. 

Tuwe makini katika kuchagua marafiki. Cha msingi sana pia, tuache tabia ya kutoa siri zetu kwa kila awaye, hata kama ni ndugu, kwani moyo wa mwenzio ni kichaka kikubwa, huweka mambo mengi ndani yake, mabaya na mazuri. Usiruhusu hiyo hali ikupate wewe, chukua tahadhari.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: