Mtoto Wa Mwenzio Mbebe Akiwa Amelala, Akiamka Huweza Kumbeba

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kwenye jamii zetu, hususani jamii za kiafrika, kusaidiana ni moja ya wajibu wa kila mtu. Pamoja na kuwa ni wajibu wetu, tunaaswa kuwa makini katika kusaidia watu. 

Watu wengi wamejitoa kusaidia watu, tena kwa moyo mkunjufu sana. Lakini inafika wakati msaada wao unawagharimu sana, hasa pale wanapokutana na maudhi toka kwa wale waliowasaidia. Maudhi yanaweza kuwa ya aina nyingi, mojawapo ni kusemwa vibaya na huyo/hao uliowasaidia. Badala ya kutoa shukurani, eti wanakusema. Wanaweza hata wakadiriki kusema umewasaidia kwa kuwapa vitu ambavyo havina thamani, ni vile ambavyo wao wanafikiri uliona huna kazi navyo, yaani ni kama vitu vya kutupa. Lakini wewe kwa moyo wako wa utu na upendo ulivitunza ili vije viwasaidie wenye uhitaji. Dharau hii huuma sana na hata kukatisha tamaa kuendelea kuwa na moyo wa kusaidia watu.

Ni mara chache sana ambapo mtu anaweza kukushukuru kwa yale uliyomtendea. Wengine hawatauthamini msaada wako katu, hata ufanyeje. Pengine ule msemo wa Tenda wema Uende zako, unaweza kufaa kwenye hili tunaloliongelea la watu kutobebeka. 

Binadamu tunatakiwa kusaidiana iwezekanavyo, pale inaposhindikana, msaada wako unapoambulia tuhuma na lawama tele, inabidi utafakari tena na tena, kama uendelee kusaidia, ama laa. Ule usemi wa Binadamu kiumbe mzito unaweza kuwa sahihi katika mazingira kama haya, mazingira ya utovu wa shukurani. Yatupasa kushukuru hata kwa kile kidogo tunachopewa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: