Uliza, Usitete

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika jamii tunayoishi, tuko katika dimbwi la kuvurugana kwa maneno na kejeli. Mivurugano hii huweza kusababisha kutofautiana kwa njia moja au nyingine. Mara nyingi, tofauti ya kipato ama maisha kati ya mtu na mtu, ndivyo huwa vyanzo vikuu vya kuvurugana ama kuleteana chuki.

Binadamu tuna tabia ya kusahau. Wengi husahau kuwa kuna Mungu ambaye humpangia kila mtu riziki yake kwa nyakati na majira yake. Kusahau huko kunatufanya tuwe tunatetana sms tunasemana vibaya. Hatuishii kutetana tu, tunatafutana kwa maneno ya kejeli na hata kumsahau Mungu. Wengine hujikuta wanaingia hata kwenye nguvu za giza ili tu mtu wamharibie mambo yake. Pale wakifanikiwa kuharibu maendeleo yake, hufurahi na hata kusherehekea huo wanaouona ni ushindi kwao. Kuteta, kudhihaki na kucheka wenzao ndio inakuwa furaha yao isiyo kifani. 

Katika hali ya kawaida, walitakiwa kuuliza chanzo cha mafanikio yake ili wajue mwenzao alifanyaje mpaka akafikia hapo alipofika. Kwa vyovyote vile, kama ilivyo kwa binadamu yeyote, anaweza kuwa alipitia magumu mengi sana kabla ya kufikia hapo alipo sasa. Ukiuliza unaweza kupata ukweli wote. Waswahili husema, ‘Kuuliza si ujinga’. Ni vema kuuliza kuliko kuteta ama kusengenya pembeni. Unaweza kunufaika na majibu utakayopata.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: