Mla Mla Leo, Sio Mla Nawe

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kwa kawaida, chakula hukusanya watu na kuwa marafiki, hata familia inapokaa pamoja na kula pamoja, mahusiano yao huimarika zaidi . Kwa maana hii, chakula hutuleta pamoja. Chakula ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu. Ili binadamu aweze kuishi, ni lazima ale. Wataalamu wanashauri binadamu ale angalau milo mitatu kwa siku. Chakula hicho kinatakiwa kiwe na viini lishe vyote ili afya ya mlaji iwe bora.

Mtu anayekula leo bila ya wewe, sio mla nawe maana hakutaka kukualika ili ule naye. Mara nyingi hutoa visingizio vingi, mfano, mtandao ulikuwa unasumbua, hali ya uchumi mbaya na visingizio lukuki. Wengine hata hudiriki kusema mwezi wa kwanza (Januari) ni dume, wakiwa na maana kuwa ni mwezi usiozalisha, bali ni mwezi wa kutoa tu.

Vinavyotoka kwenye mwezi huu ni kama ada za shule, nguo za shule pamoja na madaftari, na vikolombwezo vyote vinavyohitajika shuleni. Hali kadhalika, kwa wengi mwezi huu wa Januari huwa ni mwezi wa kulipa kodi ya pango la nyumba kwa wale wanaoishi kwenye nyumba za kupanga. Kwa kifupi, mwezi huu kwa wengi, huwa ni mwezi wa matatizo, wengi huuita ni mwezi wa balaa.

Wale wanaotoa visingizio vya mitandao, mfano, mtu mwenye sherehe tarehe 26/12 alitakiwa akualike kama siku tano kabla, lakini kwa kutotaka kula nawe siku hiyo, basi atakutafuta masaa machache kabla ya chakula siku hiyo, kisingizio kikubwa kinakuwa mtandao ulikuwa mbaya na hivyo alishidwa kukupata mapema ili akupe taarifa hiyo.

Sababu zote zile zitolewazo za kutowakaribisha ndugu, jamaa na marafiki kula pamoja, angalau hata mara moja kwa mwaka, tunachukulia kuwa ni ubinafsi wa binadamu, na si vinginevyo. Kama mtu unapanga shughuli yako ambayo itahusisha watu wengine, yakupasa kutoa taarifa mapema ili uweze kula na wenzio. Tuache visingizio.

Hali kadhalika, mwezi Januari upo kila mwaka, na kila mtu anajua matatizo ya mwezi huu wa kwanza, hivyo tunapo ulalamikia mwezi huu haileti maana yoyote zaidi ya uchoyo. Swali la kujiuliza sote ni :kwa nini tusiwe na utaratibu wa kupanga na kuweka akiba kidogo kidogo kukwepa hizo adha za mwanzo wa mwaka? Kujiandaa ni muhimu kwa kila mwanadamu. Yatupasa tutafakari!

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: