Palipo Na Chuki Ujue Wema Ulitangulia

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha tunayoishi hapa chini ya jua, ukubali usikubali chuki nyingi hutokana na wema ambao ulimfanyia mtu. Mara nyingi chuki hiyo huwa ni nzito na kubwa kuliko maelezo. Chuki inapoingia, ni dhahiri kuwa huyo mtu afanyayo hayo ujue amesahau fadhila aliyotendewa. Si ajabu hata watoto wetu tukiwaona wakisahau mambo waliyofanyiwa na wazazi wao katika kutengenezewa maisha yao. 

Palikuwa na kijana mmoja ambaye alichukuliwa na mjomba wake kuja hapa jijini Dar es Salaam. Mjomba alimsomesha kijana huyu akijua kuwa anamsaidia dada yake. Maisha ya dada yake yalikuwa duni sana kutokana na ukweli kwamba baba za watoto hawa walikuwa hawaeleweki. Kila mtoto alikuwa na baba yake. Ilikuwa ni shida tupu.

Mjomba alijitahidi kumsaidia mpwa wake kuanzia darasa la tano. Alipomaliza darasa la saba, alimpeleka shule ya private kuanza Kidato cha kwanza. Alisoma private hadi akamaliza kidato cha nne. Mjomba wake hakuishia hapo, aliendelea na kumsomesha. Alimpeleka kidato cha tano lakini kwa bahati mbaya hakufanya vizuri mitihani ya kidato cha sita.

Mjomba alikuwa na moyo mkuu, hakuchoka, alimpeleka chuo kuchukua kozi ya Manunuzi. Baada ya kumaliza alimtafutia kazi. Kijana alipopata kazi, alianza kujiinua sana na kuanza kumdharau mjomba wake. Alithubutu hata kusema kuwa mjomba wake alikuwa akimtesa sana wakati anasoma na aliongeza kwa kusema kwamba alikuwa anatumia nguvu za giza kumsumbua na kumuangamiza yeye. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba hata akikutana na mjomba wake njiani, kijana akawa hamuamkii wala kumpa salamu ya aina yoyote. 

Muda ulivyokwenda, kijana aliugua ghafla na kupoteza maisha. Swali kubwa likawa ni wapi pa kupeleka msiba? Ilikuwa ni mtihani mkubwa ambao ilibidi ndugu waingilie kati. Walimsihi sana mjomba aliokoe jahazi na walimsihii kwa kumwambia kuwa, kama ni adhabu, mpwa wake alikuwa tayari amekwishaipata. 

Mjomba wa kijana alikubali, msiba ukawa kwake. Hivyo, msiba uliondokea nyumbani kwa mjomba kuelekea nyumbani kijijini kwa mama yake kwa mazishi. Kwa ujumla, hali ilikuwa tete kwa maana hata dada mtu alikuwa anamtetea mwanae. Pamoja na yote aliyofanyiwa mtoto wake na mjomba wake, bado hakuwa na amani na kaka yake. Alikuwa akiamini maneno ya uongo aliyokuwa akiambiwa na mwanae. Wema wa mjomba ulizaa chuki isiyo kifani. 

Hebu jaribu kufuatilia kwa makini, utakuja kuona kuwa popote penye chuki wema ulitangulia. Kwa kawaida, chuki hufuta wema wote. Kwa hakika, binadamu, ni kiumbe mzito sana, tabia ya uongo ni kilema cha watu wengi. Hebu na tuifundishe mioyo yetu kuwa na shukrani na pia hebu tujifunze kusema ukweli. Mwaka 2023 uwe ni tofauti kwetu sote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: