Tenda Haki Bila Kujali Hali Ya Mtu Unayemtendea

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Siku moja kijana mwendesha baiskeli alikamatwa na Polisi kwa kosa la uzururaji. Alipofikishwa kituo cha Polisi alitakiwa atoe chochote (hongo) ili aachiwe, yule kijana alikataa kata kata. Kesho yake kijana alifikishwa mahakamani. Alisomewa shitaka tofauti kabisa na lile aliloshikwa nalo. Alishitakiwa kuwa aliendesha baiskeli isiyokuwa na taa usiku na hivyo kuhatarisha maisha. Kijana alikiri kosa na kupigwa faini ya shilingi elfu ishirini (20,000/=). Kwa moyo mkunjufu, kijana alilipa hiyo faini. 

Baadaye alienda kituoni kudai baiskeli yake. Alipofika kituoni, alimkuta Mkuu wa kituo. Alimweleza shida yake ya kwenda pale. Alimwambia kuwa alikuwa amekuja kumuona polisi aliyemkamata jana usiku. Mkuu wa kituo alimuita askari aliyekuwa anahusika na ukamataji wa kijana huyo. Mkuu wa kituo alimwamuru amrudishie baiskeli yake. 

Askari alikiri kumkamata yule kijana ila alimuomba Mkuu wa kituo aongee na kijana pembeni, fursa ambayo alipewa. Walipokuwa wawili peke yao, Askari alianza kwa kumlaumu sana yule kijana. Alimuuliza, “Kwa nini unataka kuniharibia kazi?” Kijana naye alikomaa kisawasawa kwa kusema, “Kwa nini umenibambikia kesi tofauti?” Kijana alizidi kung’ang’ania apewe baiskeli yake aliyokamatwa nayo na si vinginevyo.

Huku na huku ikabidi yule askari akatafute pesa na kununua baiskeli mpya na kumpa yule kijana. Hakukuwa na namna kwani kijana alikuwa hasikii lolote zaidi ya kudai ‘baiskeli yake’. Hatimaye alikabidhiwa baiskeli hiyo. Baada ya kukabidhiwa, yule kijana alifungua taa za baiskeli hiyo na kisha kumkabidhi askari, huku akimwambia, “Hebu chukua hizi taa, kwani ulinikamata naendesha baiskeli yangu isiyo na taa. Nisingependa kuchukua kile ambacho sikuwa nacho wakati nakamatwa”. Kijana akaendelea kwa kusema, “Napenda kukutendea haki askari wangu, nikichukua baiskeli na taa zake nitakuwa nakudhulumu”.

Ndugu zangu, mwaka 2023 ndio huu umeanza. Yatupasa tujitahidi kutenda haki bila kujali hali ya yule unayemtendea haki. Kwa nafasi yoyote uliyonayo, uwe ni Askari, Mkurugenzi, Kiongozi wa Dini au cheo chochote kiwacho, tenda haki bila upendeleo wowote. 

Tutakiane heri ya mwaka mpya 2023. Tudhamirie na tujitahidi sana kutenda mema. Tuogope dhuluma.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: