Safari Ni Fupi Sana

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Msichana mmoja aliingia kwenye basi akapata kiti akakaa. Basi liliposimama akaingia mama moja akakaa karibu naye. Yule mama akawa anamfinyafinya na kumsukuma yule msichana kwa mikoba yake mikubwa. Bwana mmoja aliona yanayotendeka. Kwa hasira akamuuliza msichana, kwa nini hasemi kitu kwa yale anayofanyiwa na huyo mama?

Binti akajibu huku akitabasamu, “Sio lazima niwe mkali na kuzungumzia kila jambo ninaloona. Safari ni fupi sana na nitateremka kwenye kituo kinachofuata.”

Haya maneno “Safari ni fupi sana” yanafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu, kwa maana tukijua kuwa safari yetu hapa duniani ni fupi, na kwamba kituo cha kushuka kipo usoni petu, hatutakuwa na sababu ya kufanya matendo maovu. Kuna mambo mengi sana binadamu tunayatenda hapa duniani ambayo inatupasa tuyatafakari kwa kina. Matendo hayo ni kama yale ya kudhulumu, kutesa watu, kuonea wengine, kujisifia kwa wenzetu kuhusu mali au madaraka tuliyonayo, kutosamehe wenzetu waliotukosea, kuwa na tabia isiyokubalika na jamii, kupuuza mambo na kutoona umuhimu wa kusali na kumjua Mungu, kutokuwa wakarimu kwa wenzetu na kukosa shukurani kwa mema mengi tunayotendewa. Kama binadamu tunafanya makosa mengi mno, makosa ambayo yametufanya tujisahau kuwa safari yetu hapa duniani ni fupi sana.

Hebu chukua muda kidogo na jiulize maswali.
Je, kuna mtu aliyekufanyia yafuatayo?

  • Amakuvunja moyo wako? Kuwa mtulivu tu ndugu yangu kwani “Safari ni fupi”
  • Amekudharau, akakudanganya? Kuwa mtulivu “Safari ni fupi”
  • Amekudhulumu?
  • Amekupora mali zako?
  • Amekuonea? Usihamaki hata kidogo, “safari ni fupi”

Je unajisikia kuwa wamesahau wema wako uliowatendea?

  • Wamekukimbia au kukufukuza?
  • Wanakudharau? Kuwa mtulivu kabisa, “Safari ni fupi”

Tuzijaze nyoyo zetu na utu, wema, ukarimu, haki, upole, huruma, upendo, shukrani, hofu ya Mungu na kuwatendea wengine mema.

Kumbuka, “Safari ni Fupi”. Mwaka 2022 umekwisha salama, ninaamini na wewe unayesoma simulizi hii, umeuona mwaka wa 2023. Jitahidi kutenda mema hapa duniani. Nakutakia heri ya mwaka mpya 2023 Safari ni fupi sana tuishi kwa wema.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: