Tufanye Maamuzi Magumu 2023 Ya Kujivua Yale Yasiopendeza

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu. Maamuzi hayo ni yale yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu.

Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake huwa magumu na huwa makali sana ambayo humfanya akose uwezo wa kunyakua chakula. Isitoshe, mdomo wake uliochongoka hupinda. Zaidi ya hayo, mabawa yake huwa mazito na hunata kwenye kifua chake, hali ambayo humfanya awe mzito wakati wa kuruka na hivyo kuwa mwenye kasi ndogo.

Katika hali hiyo ndege huyo hubakiwa na maamuzi mawili. Aidha, akubali kufa au afanye mabadiliko katika mwili wake ili aendelee kuishi kwa hiyo miaka 30 iliyobakia. Akichagua kufanya mabadiliko kwenye mwili wake itampasa kuchukua siku 150 ambazo ni sawa na takribani, miezi 5.

Katika kipindi hicho, huenda katika kilele cha mlima mrefu na kujificha katika pango. Lengo kubwa la kufanya hivyo ni kukwepa watu na wanyama wengine wanaoweza kumzuru kufika hapo. Akiwa mafichoni, huanza kujivua kucha, midomo na mbawa zake zilizozeeka huku akisikilizia na kuvumilia maumivu makali. Baada ya mabadiliko kufanyika, hurudi katika hali yake ya mwanzo ya kuweza kuruka kwa kasi na kupata chakula chake kizuri. Maisha yake huendelea hivyo mpaka mwisho wa maisha yake.

Mwaka mpya wa 2023 tayari umeanza. Sisi binadamu pia, yatupasa tufanye mabadiliko makubwa sana katika maisha yetu. Tunalazimika kujivua tabia ambazo zimeleta ukakasi ama kuwa kikwazo katika maendeleo yetu ya 2022. Tunatambua kuwa kuna tabia zingine ni ngumu sana kuziacha na pengine zitakusababishia maumivu makali, lakini waswahili husema “no pain no gain” ikiwa na maana kuwa “bila maumivu, hakuna mafanikio.

Katika mkakati wa kujivua, itakupasa ujivue baadhi ya marafiki wasiolekea unakoelekea wewe, yaani wanaoenda njia tofauti na wewe, wanaoenda na mwendo tofauti na wako. Yaani, kwa kifupi, wale ambao hamuendani kwa lolote. Katika kufanya mabadiliko hayo, itakulazimu kujivua mambo mengi tu kutoka kwenye orodha ndefu. Baadhi ya yale utakayotakiwa kujivua ni pamoja na uvivu kwani hili ni tatizo sugu kwa watu wengi ambao hutumia muda mwingi kulalamika kuhusu ugumu wa maisha wakati wamekaa tu bila kujishughulisha na kufanya kazi.

Kuna mlolongo wa mambo mengi tu ya kujivua, mathalani, uongo, mahusiano yasiyo na amani, ulevi, tabia ya kupenda kulala sana, uasherati, tabia ya kupenda kuahirisha ahirisha mipango yako bila sababu maalum, na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Ikiwa Tai anafanya maamuzi ya kubadilika akiwa na miaka 40, hata wewe bado hujachelewa, haijalishi umri uliyokuwa nao. Usiogope, fanya maamuzi sasa, fanya mabadiliko sasa, anza mwaka 2023 ukiwa na tabia mpya na mtazamo mpya. Anza safari yako mpya ya maisha ukiwa umejivua yale yote yaliyokuwa na machukizo kwa wenzio, na zaidi, kwa Muumba wako.

Mabadiliko ni muhimu, na kila mmoja wetu anatakiwa kufanya hivyo. Mungu atubariki sote katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi, maamuzi tunayoyafanya leo, siku ya kwanza ya mwaka wa 2023.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: