Ujana Ni Kama Maji Ya Moto Kwenye Chupa Ya Chai

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Sote tunaelewa matumizi ya chupa ya chai. Kazi kubwa ya chupa ya chai ni kutunza chochote kilichomo ili kiwe na hali ya joto kwa muda mrefu. Mathalani, kama mtu anasafiri, chupa hii huwa ya msaada sana. Ukiwa na chupa hii unaweza ukafika mwisho wa safari huku kilichomo ndani yake kingali bado cha moto kwa matumizi uliyokusuda. 

Ni ukweli usiopingika lazima utafika muda maji yatakuwa yamepoa na ukawa huwezi tena kuyatumia kwa matumizi uliyopangia. Usemi huu unatulinganisha na maisha yetu sisi wanadamu. Sisi wanadamu tunapozaliwa, tunafanana na maji ya moto ambayo yamechemka muda huo na kutiwa kwenye chupa ya chai. Ukifikia ujana bado maji yana motomoto unaweza kuyatumia kweye kusudio uliloyapangia. Hali hiyo ya umoto moto huanza kupoa kutokana na pilika pilika nyingi zikiandamana na mbwembwe kibao za ujanani. 

Tunapoingia kwenye utu uzima, maji ya moto kwenye chupa yanakuwa na moto kidogo sana na hata huwezi kuyatumia vile ulivyopanga. Tukizidi kwenda mbele zaidi, tukafikia hali ya uzee sana, hapo maji yanakuwa baridi kabisa kiasi kwamba unaweza kuyanywa bila wasiwasi kwa kuogopa joto lake.

Kila nikiwaza sana huu usemi ninaona kuwa una ukweli mwingi ndani yake. Niliangalia sana kwa upande wetu sisi wamama wa TEWWY. Tulianza moto moto, sasa tumekuwa kama maji ya baridi, tumepoa kabisa na pilikapilika zimepungua. Lakini tunamshukuru Mungu kwani bado kuna baadhi ya wamama wanadunda, kwa ubaridi huo huo. Wanatenda mambo makubwa sana kwenye jamii. Wanaendelea kutoa huduma za ushauri nasaha kwa lengo la kuponya roho za watu wenye uhitaji. Wanaendelea kutoa nafasi hiyo kwa kuziba pengo lililopo kati ya wazee na vijana na hali kadhalika kuziba pengo lililopo kwenye ya huduma za afya ya akili zilizopo nchini. Mungu awabariki wamama hawa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: