Furaha Yako, Machozi Yao

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kuna mwalimu alikuwa na tabia ya kumchapa mwanafunzi ambaye alikuwa mchelewaji shule kila siku. Kila akimwona mwanafunzi yule kachelewa, mwalimu yule hakusita kumchapa bakora na kisha kumsema vibaya yule mtoto darasani mbele ya wanafunzi wenzake. 

Siku moja yule mwanafunzi akawahi mapema shule. Wiki nzima mwalimu yule anamtafuta amchape bakora lakini akawa hampati kwani alikuwa anawahi. Sasa ikabidi amuulize mbele ya wenzake, “Imekuwaje, mbona siku hizi unawahi?”

Yule mwanafunzi, huku akilia akasema, “Siku zote nilikuwa nachelewa kuja shule maana mama yangu alikuwa mgonjwa sana. Ni mimi peke yangu ambaye nilikuwa naishi naye na kumuhudumia kwa kila kitu. Kila siku asubuhi nilipaswa kusafisha nyumba, kumpa dawa mama na kumuandalia hadi chakula cha mchana ndipo nije shule.” Mwanafunzi yule akahitimisha story hiyo kwa kusema, “Wiki kadhaa zilizopita mama alifariki. Ndiyo maana sasa nawahi shule”. Yule mwalimu alilia sana. Akajilaumu kwanini hakuwahi kumuuliza sababu ya kuchelewa, badala yake alimuongezea maumivu. Kwa hakika, inauma.

Katika harakati zetu za kutafuta, tuwe makini sana, tusiumize wengine na tusikubali furaha yetu iwe machozi kwa wengine. Wale tunaowaumiza, wanategemewa na wengine pia. Tena inawezekana wanategemewa sana kuliko tunavyofikiri. Mtu wa namna hiyo unapomuumiza, ujue kuwa na uwe na  uhakika kwamba umeumiza watu wengi walio nyuma yake ambao wewe huwajui. Kumbuka machozi yao hayatakuacha salama. 

Yatupasa tujitahidi sana tusiwaumize wenzetu. Hakikisha kuwa furaha yako haiwi machozi kwa wengine. Tumuombe Mwenyezi Mungu atusaidie sisi binadamu tulio na mapungufu mengi ili tuweze kuwa na utu kwa wenzetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: