Bahati Humuendea Mwenye Kuitafuta

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Dunia yetu ina mambo mengi, mazuri na mabaya. Mambo mazuri huletwa na binadamu, hali kadhalika, mambo mabaya nayo huletwa na binadamu huyo huyo. Binadamu huwa tuna tabia ya kusema sema mengi hasa kuhusu watu ambao kidogo wanajiweza. Mara nyingi watu hawa husemwa vibaya na pengine kuwaona kuwa hawakustahili kuwa vile walivyo. Maneno hayaishii hapo, huenda mbali zaidi na kusema kuwa, huyo siyo bure, ana njia zingine anazotumia kupata huo utajiri alio nao. Majungu huwa mengi, majungu yasiyo na msingi wowote.

Maneno kama hayo ni maneno ya kushindwa na kutofikiri nini kinatakiwa kifanyike, na kwa namna gani mtu anaweza kupata mafanikio. Inatupasa tujue kuwa hakuna mafanikio yanayokuja bila kujishugulisha. Hata maandiko matakatifu yamesema, asiyefanya kazi hastahili kupata ujira wowote na wala mtu huyo pia hastahili kula. 

Ukweli ni kwamba, mtu anapojishugulisha ndipo bahati huwa zinamfuata. Maisha ni vile wewe mwenyewe unavyoamua na kupanga njia za kujiongezea kipato. Tupunguze maneno, tufanye kazi na hapo ndipo tutakavyoweza kuyakabili na kuyamudu maisha. Maneno mengi yasiyo na msingi hayafanyi lolote zaidi ya kutuchelewesha. 

Kumbuka, wewe unapobwabwaja, au kuongea ovyo kuhusu binadamu wengine, wenzio wanaendelea na kupambana na maisha. Hakuna mjadala kuwa maisha ni mapambano na siyo longolongo. Zungumza kidogo, punguza longolongo, fanya mengi, tekeleza wajibu wako na hapo ndipo mafanikio yatakufuata. Mambo mazuri hutafutwa, hayajileti yenyewe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: