Leso Ni Dhahabu, Hufaa Katika Tabu

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Leso ni kakitambaa kadogo sana na mara nyingi watu huwa wanakadharau sana. Watu wengi huwa hawaoni umuhimu na kazi ya leso. Tunaweza kuilinganisha leso na binadamu ambaye hana kitu. Kwa kawaida, mtu asiye na kitu huwa ni mtu wa kudharauliwa sana. 

Ukweli ni kwamba sisi binadamu huwa tunashindwa kutambua na kuthamini umuhimu wa binadamu wenzetu hapa duniani. Ni vema ieleweke kuwa kila mwanadamu ana karama ama jambo fulani ambalo mwingine hana. Hilo halina, na lisiwe na ubishi kabisa. Ni lazima tutambue tofauti zilizopo kwani zitaendelea kuwepo daima.

Mfano ufuatao ni wa kutilia mkazo haya yanayoelezwa. Kulikuwepo na mtu mmoja ambaye alikuwa anajiona sana kwamba yeye ni matawi ya juu. Alikuwa anawadharau sana watu wengine. Ulifika wakati, jamaa huyu alikuja akafilisika vibaya sana. Hali yake ilikuwa mbaya kiasi kwamba kila mtu aliyemuona alishangaa sana na kushindwa kuamini kama kweli huyo jamaa amekuwa hivyo alivyo sasa. 

Ilitokea kwamba jirani yake ambaye mbele za macho yake alionekana kuwa si lolote wala si chochote, na kwamba alikuwa ni kama takataka kwake, ndiye aliweza kumsaidia. Wakati wa enzi za uwezo wake alikuwa hajui kama hapa mjini kuna watu huwa wanalala na njaa ama laa. Sasa hali hiyo ilikuwa inamtokea yeye. Kwa hakika dunia hii, mambo yake yanakwenda juu na chini, ndivyo ilivyo. Mambo ambayo alikuwa hayategemei katika maisha yake, ndio yalikuwa yakimtokea sasa. Watu aliokuwa akiwadharau wakati ule, ndio waliokuwa wa msaada kwake sasa. Kwa hakika hakuwahi kutegemea kuwa angekuja kuwa hivyo alivyo sasa. Alikuwa amejisahau, alifikiri maisha yangekuwa vile alivyokuwa akiyataka yeye yawe.

Kuna mengi ya kujifunza kwenye simulizi hii. Baadhi ya yale tunayoweza kujifunza ni pamoja na:

  1. Tusimdharau mtu yeyote hapa duniani hata kama wewe umebahatika kuwa nacho. Ukimuona mtu hana thamani kwako leo, ujue kuwa anaweza kuwa ndiye atakayekuja kukusaidia kesho. 
  2. Daima tukumbuke kuwa hapa duniani, kupata na kukosa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Huu ndio uraratibu na ukweli wa maisha, hivyo yatupasa tuukubali. Leo unaweza kuwa nacho na kesho pia unaweza usiwe nacho kabisa. Kupata na kukosa hakuna formula maalumu. Kupata ama kukosa ndio maisha yenyewe ya mwanadamu. 

Leso ni dhahabu, hufaa katika tabu. Kama haikufai leo kutokana na sababu mbalimbali, kesho itakufaa kabisa, hakuna wasiwasi. Binadamu tunatakiwa tusijisahau, kwani mtoaji ni huyo huyo moja, yaani Muumba wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: