Chawa Si Mzito Lakini Husumbua

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha tunayoishi hapa duniani kila mmoja anapambana na shughuli zake kwa bidii ili mradi mkono uweze kwenda kinywani pamoja na kupata mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya familia zetu. Katika kupambana huko kila mmoja, kwa wakati tofauti, hukutana na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuwa ndogo ndogo. Mara nyingi changamoto hizi zinaweza zisitiliwe maanani sana na muhusika na zikachukuliwa poa ama zikadharauliwa.

Endapo hatazidhibiti changamoto hizo tangu awali zikiwa zingali ndogo, baadaye zitaweza kuwa kubwa na nyingi. Hali kadhalika zinaweza zikasumbua na zikakufanya ushindwe kuzimudu. Mbaya zaidi hali hii ya kushindwa kumudu hizo changamoto inaweza ikakuletea msongo wa mawazo, hali ambayo inaweza kuwa tatizo kubwa kiafya, hususani, afya ya akili.

Maelezo haya yanafupishwa kwenye msemo huu, “Chawa si mzito lakini husumbua.” Msemo huu unatufundisha kuwa tuwe makini katika kutatua changamoto zozote ziwazo na inatupasa tuzishughulikie mapema iwezekanavyo na kwa wakati. Changamoto ni changamoto, ziwe ndogo ama kubwa, tusizidharau. Athari ya kudharau changamoto zetu ni kuwa na mwisho mbaya.

Hali kadhalika, usemi huu unatukumbusha umuhimu wa kuwa makini katika kushugulikia changamoto zetu mara tuzipatapo kwenye maisha yetu. Njia mojawapo ya kutatua changamoto hizo ni pamoja na kumshirikisha rafiki yako wa karibu, rafiki mliyeshibana na ambaye mnaaminiana. Siyo kila rafiki anaweza akakutunzia changamoto/siri zako.

Yatupasa tuepuke kuweka mizigo mioyoni mwetu. Inapotokea mioyo yetu kuwa imejaa mizigo ya mawazo, tuwe tayari kuitua ili kukwepa kupata matatizo ya afya ya akili, hususani, sonona ambayo imekuwa tatizo sugu kwa watu wengi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: