Mafanikio Yoyote Yanahitaji Watu

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Binadamu tunategemeana sana hapa duniani. Tukiwa katika mahangaiko yetu ya kufanya hiki na kile ili kuweza kupata mahitaji yetu, tunahitaji uwepo na msaada kutoka kwa watu wengine.

Mwanadamu akitaka kupata mafanikio yoyote, anahitaji watu. Izingatiwe kwamba, ili kutimiza ndoto yako ya mafanikio, unahitaji watu. Unahitaji watu wa aina mbali mbali na katika nyanja mbali mbali, mfano, watu wabunifu, washauri, wafadhili, wenye maono na wengineo wengi tu, kutegemeana na uhitaji wako. Lakini kumbuka kuwa moja ya siri ya mafanikio ni kutokuwaonea wivu watu waliofanikiwa. Kamwe usizungumze vibaya juu ya watu waliofanikiwa. Utakuwa unajifungia milango ya mafanikio.

Biashara zote zina mahitaji yake. Kwa mfano ukiwa na duka utahitaji wateja. Hali kadhalika, ukiwa na bus utahitaji abiria. Vile vile, ukiwa na hoteli utahitaji walaji. Hao wote ni watu. Hivyo kipato chako kinatoka kwa watu na heshima unapewa na watu. Lakini pia unahitaji marafiki wa kweli ambao watakuwa tayari kukuambia mapungufu yako kwa madhumuni ya kukusaidia, kukuimarisha na kukuinua kwenye biashara yako. 

Kuwa tayari kupokea maoni/ushauri. Usiwe na jeuri ya kujiona kuwa wewe umekamilika. Sio busara kuruhusu umimi ukutawale, ukifanya hivyo safari yako ya maendeleo itakuwa ngumu. Kama binadamu, tunahitajiana kwa kila hali, hakuna aliyekamilika.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: