Watoto Wana Haki Ya Kusikilizwa

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika kijiji kimoja alikuwepo msichana mmoja aliyeitwa Janni. akiwa na umri chini ya miaka 18 alilazimishwa kuolewa na mtu mzima anayemzidi sana umri. Mume wake alikuwa akimtesa, alimdhalilisha kijinsia, alimyima chakula na kumpiga mara kwa mara. Akitoka kulewa, hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

Tabia hiyo ilimshinda binti. Aliamua kurudi kwa wazazi wake ili kuwaeleza kinachomsibu. Cha kushangaza, wazazi wake bila huruma, walimwambia arudi haraka sana kwa mume wake. Mama alidiriki hata kumwambia mwanaye kuwa avumilie tu kwani hata yeye alivumilia hadi akamzaa yeye. Aliendelea kumwambia kuwa hayo ndiyo maisha ya ndoa, na kwamba ndoa ni ndoano.

Baada ya muda Janni alijaliwa kuzaa mtoto, lakini mateso yaliongezeka mara dufu. Ilimlazimu achukue hatua madhubuti. Alifungua kesi dhidi ya mume wake wakiwemo wazazi wa pande zote mbili. Mume pamoja na wazazi wake walipewa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi minne. Wazazi na mume walikasirika sana kwani waliona kuwa wamedhalilishwa.

Kutokana na maisha kuwa magumu, ilibidi Janni ajiongeze ili kupata mahitaji yake na ya mwanaye. Janni alienda kugonga kokoto lakini kwa bahati mbaya sana jiwe lilimgonga usawa wa bandama na akalazimika kufanyiwa operesheni na kuondolewa bandama yote.

Janni aliwalaumu sana wazazi wake na akasema laiti wangelimsikiliza mateso yote hayo yasingemkuta. Janni ana uchungu sana kwa yaliyompata na anashauri wazazi wawe wanawasikiliza watoto wao mapema. Inatupasa tuzingatie kuwa siyo kila lalamiko litokalo kwa watoto halina msingi ama halina maana na kuona kuwa halistahili kusikilizwa. Kuna baadhi ya malalamiko mengine ni ya msingi na mengine yana busara ndani yake. 

Janni anatoa ushauri kwa wazazi wote kuwa wawe makini na wawe na masikio ya kusikia masuala yahusuyo watoto wao. Dharau ya kuona kuwa watoto hawana la maana la kuzungumza ama kushauri, linaweza likagharimu maisha yao na baadaye ikawa “Majuto ni Mjukuu” kwa upande wa wazazi. 

Tukumbuke kuwa kila mtu ana haki ya kusikilizwa, hususani watoto, ambao sote tunajua kuwa wanapoteza mwelekeo kwa sababu nyingi, moja kubwa ikiwa ni kutosikilizwa👂🏽na wazazi na hata jamii kwa ujumla.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: