Upendo Ni Mbegu Njema

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha usijipe tabu kwa kujiuliza maswali ya “kwani nini fulani hanipendi”. Ukichukua muda ukawaangalia hao unaojiuliza kwa nini hawakupendi, utakuta hata wao wenyewe hawajipendi! Wewe kuwategemea wakupende wewe ni kupoteza muda wako. Upendo unatakiwa kuanza na wao wenyewe kwanza, ama sivyo inakuwa siyo rahisi kuugawa kwa watu wengine.

Hivyo ili kujiepusha na maumivu kutoka kwa watu, inafaa uwachukulie watu kama walivyo na sio kama wewe unavyotaka wawe. Kuna watu hawawezi kuwa kama unavyotaka wewe, hata iweje. Kumbuka sio kila utakayempenda, utakayemjali na kumthamini naye atafanya vivyo hivyo kwako.

Punguza matarajio kutoka kwa watu (lower your expectations from people). Ukiweza kuwapenda watu fanya hivyo, lakini usifanye kwa matarajio ya kupokea upendo kutoka kwao. Siyo ajabu kumpenda mtu kupindukia lakini wewe usipokee ulichokitarajia kutoka kwake. Ubaya wa mtu mmoja usiondoe tunda la roho la upendo ndani yako. Upendo ni mbegu njema sana, endelea kuipanda kila uchao. Kumbuka, upendo hutuweka karibu na Muumba wetu. Kuna raha katika kupenda na vivyo hivyo, kuna tabu katika chuki. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: