Dunia Ya Sasa Imebadilika

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Zamani tukisoma shule, enzi za miaka 1963 hivi, binti mdogo alipendwa na kijana wa kiume wa darasani kwao. Wote walikuwa darasa la nne. Binti alimkataa kwa nguvu zake zote lakini kijana hakumwelewa, kwa maneno mengine, somo halikupanda sawasawa kichwani.

Kijana yule hakuridhika na majibu ya huyo binti. Hivyo alidiriki kumwandikia barua ya mapenzi binti yule. Msichana alifurahi sana kupata barua hiyo kwani alikuwa anataka kupata uthibitisho wa kupeleka suala hilo kwa walimu. 

Pamoja na kwamba msichana alikuwa rafiki yetu, hakutuambia azma yake ama kile alichokuwa amepanga kufanya. Kwa kuwa alikuwa amekwisha mwambia kuwa hataki mahusiano ya kimapenzi na mvulana yeyote na kwamba alikuwa hajui mambo hayo, aliamua, bila kusita, kuipeleka barua hiyo moja kwa moja kwa mwalimu wake wa darasa. 

Baada ya mwalimu kupata maelezo na kuisoma barua hiyo, mvulana huyo alipewa adhabu kali, na kuchapwa viboko mbele ya shule nzima. Aliambiwa pia kuwa adhabu yake nyingine ni kuwa atakuwa chini ya uangalizi maalumu kuhusiana na tabia yake hiyo.

Zamani, enzi za usichana wetu, ilikuwa ni kawaida kwa wanafunzi kushitaki kwa walimu tabia mbaya za wanafunzi kujihusisha na mapenzi. Hali kadhalika, mwalimu alikuwa anaheshimika sana na alikuwa na hadhi kubwa katika kumaliza kesi zilizoendana na nidhamu. Walimu walikuwa wanawalinda sana wanafunzi wao na kuwaasa wawe na tabia nzuri, na kwamba wajihusishe na masomo zaidi na si vinginevyo. 

Sasa hivi, hali imebadilika sana. Walimu wa sasa ni tofauti na wale wa zamani. Wanafunzi ndio usiseme, wanarubuniwa na vitu vidogo vidogo kama vi chips mayai, kupewa usafiri wa bure na mengineyo mengi. Ustaarabu wa kukataa dezo ulikuwepo zamani. Wanafunzi mabinti wanadanganyika sana. Na pia wengine wanapotishiwa kuwa watauawa kama watasema ukweli kwa mtu yeyote, wananyamaza. Matokeo yake wamekuwa wanafanyiwa vitendo vya unyanyasaji kama vile kulawitiwa, kubakwa na vitendo vingine vingi viovu. Kwa ujumla, jamii imeharibika. 

Tunawsihi watoto wawe makini na yale wanayotendewa na pia wawe wazi kwa walimu wao na hata kwa wazazi wao ili matendo haya ya kikatili yapungue na hatimaye kuisha kabisa. Kukaa kimya kwa kuogopa hakusaidii kabisa. Kwa kuwa wa wazi, na kwa jamii kuwajibika, mimba za utotoni zitakwisha ama kupungua kwa kiasi kikubwa. 

Mabinti zetu, tunawaasa kuwa kuishi bila mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo inawezekana. Amua sasa!!

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: