Siku Ya Kufanikiwa Ufurahi Na Siku Ya Mabaya Ufikiri

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Unaweza kupitia changamoto fulani katika maisha yako na kila ukitafuta njia za kujinasua huzioni. Wanaokuzunguka hawakupi usaidizi. Hata kama ni wale ambao ulikuwa unawategemea, nao huwaoni kabisa. Katika hali hiyo usichanganyikiwe na wala usifanye haraka na kusema maneno mengi ya kukata tamaa. Unatakiwa unapokutwa na mabaya ufikiri na jiulize kwa nini hayo yanakutokea. Inawezekana hayo yanayotokea, yana sababu, na pengine ni kukutoa hapo ulipo. Waswahili hunena, kila jambo lina ushuhuda wake. Tatizo letu sisi binadamu tunataka hali tuliyo nayo leo na kesho iwe vile vile au hata zaidi. 

Kumbuka kila jambo lina gharama yake na kama linakuwa zito sana kwako, tafuta njia ya kulitua. Yakupasa upate ujasiri wa kuweza kumweleza mtu unayemuamini. Unapopatwa na changamoto. Itabidi ufanye hivyo ili isije ikafikia hatua ukatamani kuuondoa uhai wako bure. Uhai wako ni wa thamani sana, huna mamlaka ya kuuondoa. Majibu ya changamoto ni kutafuta ufumbuzi na siyo kujiua ama kuua. 

Changamoto zipo na zitaendelea kuwepo, tukubali ama tusikubali. Tafuta ufumbuzi wa changamoto zako na ukipata majibu, yafanyie kazi nawe utashinda. Siku ya kufanikiwa furahi na siku ya mabaya fikiria namna ya kupata ufumbuzi. Changamoto ni mtaji.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: