Chapa Kazi, Sio Mkeo

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Msemo huu unalenga kwenye matukio yanayoendelea hapa nchini na nchi nyingine za Kiafrika. Ni jambo la kusikitisha sana kuona akina baba wengi wanasahau wajibu wao wa kulea familia. Kutokana na hali hiyo ya akina baba kujibweteka, akina mama wamekuwa wakijituma kwa njia mbalimbali ili familia zao ziweze kupata chakula, mavazi na hata karo za shule kwa ajili ya watoto. 

Shughuli nyingi za akina mama hufanyika hadi usiku na wengine mpaka mchana kwa kuchelewa. Kitendo cha kuchelewa huwakera akina baba wengi ambao hushindwa kuvumilia. Wengine huwa na hisia mbaya juu ya wake zao, huwafikiria kuwa labda pengine walikuwa na mipango na wanaume. 

Kutokana na hisia hizo, huishi kwa kutembeza kipigo na kuleta tafrani ndani ya nyumba. Cha kushangaza zaidi, mwanaume huyo anapompiga mkewe, yeye mwenyewe anakuwa hajaleta chochote nyumbani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Tegemeo lake kubwa ni kile kitakacholetwa na mke wake, ambaye kuchelewa kurudi anafikiriwa vibaya. Mara nyingine, mwanaume huyu hata ndani hatoki, kazi yake ni kula na kulala. Pamoja na uvivu wake huo, wivu wake dhidi ya mke wake unakuwa ni balaa. 

Hapo ndipo maswali mengi tunajiuliza, “kama ni mwanaume kweli si aende akachape kazi? Kwa nini amchape mke wake ambaye ndiye mleta riziki ndani ya nyumba?” Mke wake ndiye anayemlisha, anamvisha na kumfanyia kila kitu. Wanaume wenye tabia ya namna hii inawapasa watafakari mienendo yao. Je kuwa mume ni tiketi ya wewe kusambaza kipigo kwa mke wako? Hebu tujiulize kidogo, majukumu ya baba mwenye nyumba, haswa ni yepi? Hivi inaingia kichwani kweli  kumpiga mkeo anayekupa hadhi ya kuitwa baba mwenye nyumba kwa kuleta mahitaji ya hapo nyumbani? Baba mwenye nyumba, kufuatana na mila na desturi, anatakiwa kulisha familia na si vinginevyo. Jina la ‘baba mwenye nyumba’ ni jina kubwa sana kwenye jamii inayomzunguka. 

Ombi langu kwa wanaume ni kwamba wawaheshimu wake zao maana ni wasaidizi wao ambao wanastahili kupendwa na siyo kupigwa. Ili familia ziwe na amani zinahitaji mshikamano, hapo ndipo baraka za Mungu zitakavyoweza kuingia ndani ya nyumba zao.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: