Tafakari Kwanini Wakati Mwingine Unashindwa

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha tunayoishi, kunakuwa na muda ambao mtu unajikuta unashindwa kutimiza malengo uliyokuwa umejipangia. Wakati mwingine unajikuta kuwa kuna jambo ambalo ulijua kuwa ulikuwa umeshinda. Lakini ukiangalia, unakuta kumbe jambo lile halikwenda kama ulivyotaka ama ulivyokuwa umepanga.

Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuwa yamesababisha hali kuwa hivyo. Kwanza kabisa ni utayari wako katika hilo jambo. Maana kama ulikuwa na utayari hauna sababu ya kukata tamaa, unatakiwa kujaribu tena na tena. Usiangalie yaliyopita ambayo yanaweza kuwa yalisababisha kushindwa. Yaliyopita, yamepita angalia ya leo uliyokuwa nayo, yale yajayo hayako ndani ya uwezo wako. Yakupasa ujitambue kwanza, ujijue wewe ni nani na kwamba una jambo kubwa ambalo mwingine hana. Jitambue kuwa wewe ni kiumbe wa thamani sana, na ni wa kipekee. Usijilaumu kuwa labda umechelewa, bali jua kuwa kuna wakati na majira, vyote vinakuja. Usikae na jambo moja kwa muda mrefu ukisononeka. Tambua kuwa lipo jambo mbele yako ambalo mwingine hana. Hali ya kusononeka itakufanya uanze kushindana na watu wengine ambao wamefanikiwa.

Unapoona mafanikio ya wenzio yakupasa utambue kuwa na wao wametoka mbali hadi wakafikia hapo walipo. Kila unalolitenda, jua kwamba kama likishindikana leo, kesho linaweza likapata ufumbuzi. Yatupasa kujiamini na kutia bidii kwa yote tunayotenda.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: