Mwenda Kasi, Mngoje Achoke

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Watu husema kuwa anayekwenda mbio, usishindane naye kwani utajichokesha bure. Ukimuona mtu wa namna hiyo, yakupasa umngojee mpaka achoke, aishiwe pumzi ya kuweza kuendelea mbele. Akifikia hatua hiyo ya kuchoka, wewe unaweza kumpita kwa urahisi sana.

Msemo huu hutumiwa kuonyesha kwamba mtu yeyote mwenye papara na vishindo vingi, asiye makini wala mpangilio katika utendaji wa mambo yake huwa hakawii kuchoka na hivyo kukosa kufikia malengo yake. Uzoefu unaonyesha kuwa watu wa namna hii, mara nyingi hushindwa na kuishia njiani bila kukamilisha yale waliyojipangia. Tunashauriwa kuwa tukikutana na watu wa aina hii, tusipoteze muda wetu kuwafuata ama kushindana nao. Inakupasa wewe uendelee na mwendo wako ule ule, na hatimaye, atakapochoka, utampita.

Hali kadhalika, usemi huu hutumiwa kutufunza kwamba, tunapomuona mtu ameshikilia ama kuling’ang’ania jambo ambalo si zuri, na akawa hasikii wala kupokea ushauri kutoka kwa mtu yeyote yule, tusipoteze muda wetu kumuasa kwa wakati huo kwa maana hatakusikia kwani ndivyo alivyo. Uking’ang’ania kutaka kuendelea kumsemesha utakuwa unapoteza muda wako bure. Itakubidi umngojee mpaka litakapompata la kumpata au hadi atakaposhindwa. Hapo unaweza ukasema naye na katika hali ya kawaida, anaweza akakusikia na kukuelewa. Hii ina maana kuwa kila jambo na wakati wake.

Tujifunze namna ya kuishi na watu wa aina zote, hii ni pamoja na waenda kasi, kwani kila mmoja wetu yuko tofauti na binadamu mwingine.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: