Tuna Sababu Ya Kumshukuru Mungu

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kwenye maisha unaweza kupitia nyakati ngumu sana ambazo kiukweli ukitazama huoni utatokaje. Ni nyakati ambazo unakuwa hujui umeingiaje na pia ukijitafakari huoni utatokaje.

Ni nyakati ambazo hakuna anayekuelewa ,ni nyakati ambazo yumkini hata watu wako wa karibu wanajitenga na wewe, unajaribu kuwaza kwamba labda umewakosea lakini ukijitafakari huoni hata kosa lako ni lipi.

Ukweli ni kwamba nyakati hizo zipo na humpata karibia kila mtu. Kuna nyakati unategemea kupata msaada kutoka kwa wanadamu, lakini ukiangalia huoni kama kuna yeyote anayeweza kukusaidia. Kuna wakati, msaada kutoka kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki utafika mwisho, ila Mungu pekee atasimama na wewe. Hivyo basi una sababu ya kumshukuru Mungu kabisa. Mahali ulipo na namna ulivyovuka ni Mungu pekee anakuwa amekusaidia. Mungu wetu mwenye upendo yuko nawe, daima hatakuacha na wala hatakupungukia.

Uliposhindwa mwambie, ulipochoka mwambie. Anajua yote unayoyapitia, yote unayotaka. Anajua haja za moyo wako. Kinachotakiwa, ni wewe tu kumjulisha ili akuvushe. Kumbuka, wewe ni wa thamani sana kwa Muumba wako. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: