Nidhamu Na Taratibu Katika Maisha

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha watu wanaofanikiwa ni wale wenye nidhamu ama taratibu za maisha katika mambo yao. Wengi ambao unaowaona leo wamefanikiwa, ukiwafuatilia kwa karibu unaweza kugundua kuwa mafanikio yao yanatokana na nidhamu kubwa waliyokuwa nayo kwenye maeneo mbalimbali, mathalani,

1. Nidhamu ya muda 

Watu wenye nidhamu ya muda mara nyingi hujua nini wafanye na wakati gani. Watu hawa huwa makini sana na ratiba waliyojiwekea na huhakikisha kuwa haiingiliwi na jambo jingine lolote ambalo haliko kwenye ratiba ya siku hiyo. Watu wa aina hii hufanya kazi kwa mpangilio maalumu, mathalani, ukitaka kukutana nao inabidi uwaombe wakupangie muda na siku ya kukutana nao. Muda wao mwingi tayari unakuwa umeishapangiwa mambo mengine ambayo hawawezi kuyapangua.

2. Nidhamu ya fedha

Nidhamu hii ni muhimu sana katika kupiga hatua kiuchumi. Watu wengi waliofanikiwa katika maisha huwa na mpangilio wa matumizi ya fedha hata kabla fedha yenyewe haijafika kwenye mikono yao, wanajua nini wataifanyia fedha hiyo endapo itabahatika kuingia mikononi kwao. Ni kawaida ya walio wengi kuipangia fedha ikiwa mikononi mwao. 

Madhara ya kusubiri fedha ifike ndio uipangie matumizi utajikuta unaiweka fedha hiyo kwenye jambo ambalo siyo la manufaa kwako, linakuwa ni jambo la kukurupuka tu, ili mradi fedha ipo. Kwa mfano unaondoka nyumbani na fedha ambayo hujaipangia matumizi yoyote, endapo utakiona kitu chochote humo njiani unamopita, utanunua. Wanawake tulio wengi ni malimbukeni wa hii tabia. Mama au binti akiona nguo hata kama hakupanga kununua, atataka kuinunua, inaweza pia kuwa kitu chochote, mfano, mkoba, mara viatu, visheti, karanga nk. Pamoja na tamaa tulizokuwa nazo akina mama, yatupasa kuwa makini kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya kutumia fedha. Ni lazima ujiuluze …… je hicho unachotaka kukinunua kilikuwa kwenye mpango wako?

Hali kadhalika , madhara mengine ya kutokuwa na nidhamu ya fedha ni kununua vitu vingi ambavyo baadaye hutakuja kuvitumia. Binadamu huwa hatukosi maneno ya kujitetea pale unapokuwa umetumia fedha bila mpangilio. Hatuchelei kujitetea kwa kusema…… niliona ni bei rahisi, nimekipata kwa bahati kwani nilikuwa na haja nacho tokea zamani nk…. swali ni ….je hicho kitu kilikuwa ndani ya mpango wa matumizi ya fedha hizo?

Jiulize ni vitu vingapi ulivinunua, vimejaa ndani mwako lakini huvitumii na huna mpango wa kuvitumia si leo wala kesho? 

3. Nidhamu ya mahusiano hususani kwenye ndoa 

Kila mhusika kwenye ndoa ni lazima asimamie ndoa yake. Mfano Neno linasema ndoa na iheshimiwe na watu wote. Je wewe mwenye ndoa mwenyewe unaiheshimu ndoa yako? Au unachukulia ki urahisi rahisi tu na hauoni kama ni kitu cha thamani hata ukikipoteza itakuwa sawa tu? Yatupasa tujiulize:

– Je tuna nidhamu/taratibu mbalimbali kwenye maisha yetu ambazo tunazitii na kuziheshimu?

– Ni nidhamu/taratibu gani tulijiwekea na baadaye zikatushinda? 

Kwa nini?

Leo amua kujiwekea nidhamu/taratibu ambazo hazitamruhusu yeyote kuziingilia na kukuondoa kwenye mstari 

Maisha bila nidhamu/taratibu huchelewesha mafanikio. Yatupasa tuzingatie hayo kwani ndio msingi wa maisha ya mwanadamu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: