Chezea Mshahara, Usichezee Kazi

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Msemo huu siyo mpya katika masikio ya wengi. Ukitafakari kwa undani, msemo huu una mafunzo ndani yake. Ni kweli kuwa unapokuwa na kazi kama mtumishi, lazima uwe makini na majukumu na taratibu za kazi, kwa kufanya hivyo ndivyo unavyozidi kujenga uaminifu na kudumu kazini. Pia shirika nalo linafaidika na kukua kutokana na uaminifu wako. 

Mshahara ukiishaingia kwenye akaunti yako, unaweza kuutumia vile utakavyo, wewe ndiye mmiliki, hakuna atakayekuuliza. Kwenye kazi lakini ni lazima ufuate sheria na kanuni za utumishi. Mshahara ni matokeo ya kazi unayoifanya kwa uaminifu. Mfano mwingine ni pale unapotaka kufanya biashara na ukachukua mkopo mahali. Hapa mkopo unakuwa ndio ajira yako kwa sababu ndio unaokuwezesha kujiajiri. Yakupasa uutumie mkopo huo vizuri kwa shughuli iliyopangwa na si vinginevyo.

Kwa kawaida, mikopo inapaswa kurejeshwa kwa wakati kama inavyotakiwa na chombo kilichokukopesha. Kwa hiyo ukiuchezea mkopo hutaweza kuzalisha matunda tarajiwa na mwisho utashindwa kurejesha mkopo. Ni BUSARA, unapoingia mkataba na mtu binafsi au kampuni au popote pale kwa ajili ya utumishi, uwe mwaminifu katika kutekeleza majukumu maana ndicho kitakachoifanya kazi yako idumu lakini pia na hilo shirika liweze kuwa endelevu kwa faida ya vizazi hata vizazi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: