Sio Kila Rafiki Ni Wa Kweli

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Ni kawaida kabisa katika maisha yetu kuwa na rafiki ambaye unaweza hata kumuita ni ndugu yako kutokana na vile mlivyoshibana. Lakini kuna rafiki ambaye anaweza kuwa ni mwiba wenye sumu kali kwako. Siyo ajabu!

Palikuwa na dada mmoja ambaye alikuwa na mume wake. Alikuwa na rafiki ambaye ni wa kabila moja na yeye. Katika urafiki huo wakawa wanaelezana habari zao zote pamoja na za michepuko yao. Kumbe mwenzake alikuwa anamzunguka, alikuwa anatembea na mume wake na hivyo kumueleza yote aliyokuwa akiyajua kuhusu rafiki yake. Hebu fikiria, ni mangapi walielezana au kufanya kwa pamoja kama marafiki!Mungu tu anajua. 

Ilitokea kuwa habari zake zote chafu zilikuwa zinamfikia mume wake kila alipozisimulia kwa rafiki yake. Jinsi muda ulivyozidi kwenda, mwanamke huyo mwenye mume, alianza kuona mabadiliko ya tabia kutoka kwa mume wake. Mume alianza kurudi nyumbani saa anazozitaka yeye, hata usiku wa manane. Kumbe alikuwa akishinda kwa yule rafiki wa mke wake. 

Hatimaye, wasamaria wema walimtonya bibi huyu. Aliposikia, akaanza kumuwakia mume wake, akawa kama mbogo aliyejeruhiwa. Kwa sauti ya hasira, alimuuliza mume wake sababu za kuchelewa kurudi nyumbani. Mume naye, kwa sauti iliyojaa jeuri na kebehi, alimwambia yote waliyokuwa wanafanya na kuongea na rafiki yake kipenzi. Alimfungulia kitabu kizima bila chenga, wala kuficha lolote. Mke wake hakuamini aliyoyasikia. Kama kuongeza chumI kwenye kidonda, mume alithubutu kumwambia kuwa yule rafiki yake sasa ni mke mwenzake. 🙆🏽‍♂️

Mama wa watu alichanganyikiwa, akaamua kurudi kwao Musona. Kwa kufanya hivyo ndio alikuwa anahalalisha mahusiano ya hao wawili. Bi mdogo alifikia hatua hata ya kujengewa nyumba na hivyo akaishi raha mstarehe na bwana yule. 

Kwa bahati nzuri yule mke mkubwa alikuwa na watoto. Mama ni mama, watoto walimrudisha mama yao Dar, wakamjengea nyumba ya kuishi huko Kigamboni.

Simulizi hii inatufundisha kuwa, mara nyingi, adui yako ni yule yule unayekula pamoja naye. Hebu fikiria jinsi walivyokuwa wakimegeana siri za uvunguni kabisa mwa roho, siri ambazo zimekuja kuanikwa hadharani kwa mtu ambaye hakutakiwa kuzisikia asilani. 

Hii ni simulizi ya ukweli kabisa, ilitokea Kigamboni. Kutokana na simulizi hii, tunajifunza kuwa makini sana na marafiki, wengine sio wazuri. Hali kadhalika, hatutakiwi kumwamini rafiki kwa kumumegea mambo yako ya siri. Tuchague mambo ya kumwambia mtu/rafiki. 

Lakini pia kama mama mwenye familia, mume na watoto unaona ni ufahari kumweleza rafiki yako mambo ya kuwa na ‘vijibwana vya nje ya ndoa’, unajivunjia heshima yako kwa watoto na jamii inayokuzunguka. Ona sasa huyu mama alivyoponzeka kwa kumueleza ‘rafiki’ yake huyo feki na hayo yaliyompata. Wahenga walisema, ‘Kikulacho ki Nguoni Mwako.’ 

Pamoja na yote, sote, wake kwa waume, twapaswa kuwa waaminufu kwenye ndoa zetu. Michepuko mwisho wake huwa mbaya na hatari. Tulinde heshima zetu, mabibi na mabwana.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: