Hakuna Siri Ya Watu Wawili

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Ni kweli kabisa hakuna siri ya watu wawili. Katika maisha yangu na sehemu zote nilizopita, shuleni, chuoni, kazini na mpaka kanisani, sijawahi kumuona mtu mwenye moyo na uwezo wa kutunza siri, iwe yake mwenyewe ama ya mwenzake. Mtu anaweza akakufuata na kukueleza jambo la mtu mwingine na kisha anamalizia kwa kusema, “yaishie hapa hapa, chonde, usimwambie mtu.”

Baadaye na wewe nawe unahamia kwa mtu mwingine kwa kudhani kuwa, ukimwambia siri hiyo utaonekana wa maana sana na kwamba utaonekana unajua mambo/siri nyingi za watu. Mzunguko utaendelea kuwa hivyo hadi kilichokuwa kinatakiwa kiwe siri, kinaanikwa peupe mbele za umma

Jamani, napenda ieleweke kuwa, hata kati ya mke na mume hakunaga siri. Mahali popote pale ambapo pana watu wawili, pengine inaweza ikatokea, mume akamwambia rafiki yake, na mke naye halikadhalika akafanya vivyo hivyo. Mwishoni, utaona kuwa, ile iliyotakiwa kuwa SIRI imetapakaa kila kona. Je hapo kunakuwa na siri tena?

Hata watumishi wengine wa Mungu wanapoombea waumini wao hutoa siri za watu. Pale wanapotumia shuhuda za watu bila kibali cha wahusika wanakuwa wametoa siri, hili nalo ni kosa kubwa. Huenda wanafanya hivyo kwa makusudi ama kwa kutokujua.

Ni vigumu kwa binadamu kutunza siri, mwenye uwezo huo ni Mungu peke yake. Hii ina maana kuwa ukimwambia mtu jambo lako ambalo unaliona kuwa ni la siri, jua wazi kuwa siku moja litatoka nje na utalisikia mahali pengine. Endapo itatokea hivyo, usipate shida, usishangae wala kukasirika maana ungetaka lisijulikane ungekaa nalo mwenyewe.

Usemi wa Hakuna Siri ya Watu Wawili ni sahihi na kweli kabisa katika maisha yetu. Yale tunayotaka yabakie vifuani mwetu, basi na iwe hivyo. Siyo kila jambo lako ulianike nje kwa kumwambia kila mtu kama siri. Binadamu hawana uwezo na vifua vya kutunza siri. Siri yako kaa nayo mwenyewe la sivyo usiiite kuwa ni siri kama utaitoa kwa mtu mwingine, itatoka hadharani siku moja, uwe na uhakika na hilo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: