Ukibebwa, Bebeka

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Matumaini ya mama siku zote anapombeba mwanae ni kuwa atabebeka na baadaye atakuwa wa msaada kwake. Fuatilia haya mazungumzo kati ya mama na mwanaye:

Mtoto: (Akiwa kidato cha sita), Mama hapa shuleni nimefukuzwa kwani ada inahitajika.

Mama: Mwanangu hapa nilipo sina hela, ndiyo nimetoka kijiji jirani kuazima pipa la kukoroga pombe ili nipate ada yako. Kazana tu kusoma mwanangu.

Mtoto: Sawa mama naomba nitumie na hela ya matumizi.

Mama: Sawa mwanangu.

Mtoto: Mama nashukuru kwa ada nilipata lakini nitumie hela ya mtihani inahitajika haraka kwa ajili ya usajili.

Mama: Mwanangu kwa sasa sina hela, jana tu tumelalia uji, ila nitajitahidi nikakope kwa Mzee Kopesha ili baadaye nikalipe kwa kufanya palizi shambani kwake. Lakini Mwanangu nakusihi sana usome kwa bidii uje utukomboe na sisi baadaye.

MTOTO AFAULU KWENDA CHUO

Mtoto: Mama yangu, muda wa kwenda chuo umewadia nami sijapata mkopo wa kunisaidia chuoni. Nitafanyaje?

Mama: Mwanangu, kama nimeweza kukusomesha kote huko kwa kupika pombe za kienyeji nitashindwaje? Niko tayari kuendelea kupika pombe na kukopa ili mradi usome.

MTOTO AMALIZA CHUO, APATA KAZI NZURI.

Mama: Mwanangu, mbona siku hizi hunikumbuki? Hata hunipigii simu tena, kwa nini?

Mtoto: Mama kazi ni nyingi sana. Nilikuwa Zanzibar kikazi ndio kwanza nimerudi mama. Hebu nisamehe bure mamangu.

Mama: Kwani huko Zanzibar kuna mitandao tofauti na huku bara mwanangu?

Mtoto: Hapana mama, isitoshe mkweo ni mja mzito hivyo namuhudumia wakati wote nikitoka kazini.

Mama: Mdogo wako amefukuzwa shule hana ada. Niliuza pombe nikapata hela kidogo akaenda kulipa lakini haikutosha, kafukuzwa tena.

Mtoto: Mama hivi bado unatengeneza hayo mapombe yako ya kienyeji tu? Kwani biblia inasemaje kuhusu pombe. No, mama hapo unanikwaza nikueleze ukweli kabisa.

Mama: Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza hizo hizo pombe za koenyeji . Lakini kama ungetuma pesa ukanipunguzia huu mzigo wa kusomesha mimi ningeacha kupika pombe hizo.

Mtoto: Ningekutumia mama lakini samahani kwa sasa nakimbizana na ujenzi wa kagorofa kangu, hata nikikuahidi sasa nitakudanganya tu kwani nilichukua mkopo benki hivyo nakatwa hela kubwa sana. Mama nitakupigia baadaye kuna rafiki yangu ananipigia.

SIKU NYINGINE TENA

Mama: Hamjambo wanangu? Nataka nije kumsalimia mjukuu wangu huko mwezi huu.

Mtoto: Mama kwa sasa hatuna hela kabisa, mjukuu wako kwa mwezi huu mmoja tu ametumia kama milioni mbili. Isitoshe, tunaenda likizo Uingereza kusherehekea bethidey ya mtoto, wetu, labda tukirudi ndo tutaangalia kama unaweza kuja kutusalimia.

Hii ndiyo ilikuwa hali halisi kati ya mama na mwana.

JE, VIJANA TUNAJIFUNZA NINI?

  1. Tukibebwa tubebeke
  2. Tuwe na heshima kwa wazazi.
  3. Wazazi ndiyo kioo au chanzo cha maisha yetu ya baadaye
  4. Turudishe wema kwa wema na siyo wema kwa mabaya na dharau.
  5. Tukumbuke tulikotoka hata kama kuna hali mbaya kiasi gani.
  6. Hapa duniani kuna kupanda na kushuka.
  7. Tusiwe malimbukeni wa maisha kwani utandawazi upo siku zote twende nao taratibu. Tutafika tu.

WOTE TUJIULIZE

  1. Je tuna vijana wangapi wa aina hiii majumbani mwetu na hata nchini kwetu? 🤷🏽‍♂️
  2. Tufanye nini ili kuokoa hili jahazi linalozama?

TAFAKARI 🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: