Kaa Karibu Na Aliyefanikiwa

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha ya kawaida tuna tabia ya kumuogopa mtu aliyefanikiwa kimaisha. Pengine tunaona kuwa tunajidhalilisha ama labda huyo mwenye mafanikio atakataa kutusaidia. Lakini ukweli ni kwamba, hatutakiwi kabisa kumuogopa mtu kama huyo, yatupasa tuwe naye karibu ili kuweza kuzichota busara zake. Kwa kumuogopa tutakuwa tunajikosesha mengi, kama vile kujua siri ya mafanikio yake. Tukiwa karibu naye tutaweza kufahamu jinsi alivyopambana na vikwazo hadi kufikia hapo. Kama ni mtu mstaarabu na mwenye moyo wa uzalendo, atakuambia mapito aliyopitia, jinsi alivyoanza, vikwazo alivyopata na jinsi alivyovitatua na hata kufikia hapo alipo.

Pengine kuna jambo ambalo wewe unakusudia kulifanya, lakini kila ukiangalia unaona hupati majibu au unapata majibu ya kukatisha tamaa, majibu ama njia zisizoeleweka. Unafiki a hatua ya kukata tamaa. Pengine ungemshirikisha mtu mwenye mafanikio ungeweza kupata ufumbuzi wa namna ya kuanza na hali kadhalika kukabiliana na vikwazo mbali mbali.

Ni kwa maana hiyo tunashauri kuwa tusimuogope mtu aliyefanikiwa. Kila
mtu hupitia vikwazo katika kufanya jambo, na hata yeye huyo unayemuogopa kuna mahali alilazimika kutafuta ufumbuzi hadi akafanikiwa. Endapo atakushirikisha njia alizopitia, utapata faida na hatimaye na wewe kuweza kufanikiwa. Kuwa jasiri, USIOGOPE.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: