
Simulizi …
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Katika maisha yetu tunapitia changamoto, shida na matatizo mengi ya hapa na pale. Mapito haya ni ya kawaida kabisa. Lakini kuna watu wengine ambao wamejenga tabia ya kujirudia rudia, mathalani, kuomba omba hata pale kile aombacho kipo ndani ya uwezo wake. Mazoea hayo ya kuomba yanajengeka zaidi na zaidi hadi hali hiyo inakuwa haivumiliki mtena.
Suala la kukopa pia mtu anapopata shida sio vibaya ni jambo la kawaida ili aweze kujitoa katika changamoto aliyokuwa nayo. Lakini wengi wetu tukianza kukopa ndio inakuwa tabia, leo kwa huyu, kesho kwa yule. Wakati mwingine mtu anaendelea kukopa tu bila hata kulipa madeni ya nyuma. Malimbikizo yanakuwa makubwa kiasi cha kumchanganya mkopaji.
Kuna tabia nyingine ya mtu kufanya makosa kila siku na mara nyingi makosa yanakuwa ni yale yale, yanajirudia. Hali hii nayo haikubaliki, siyo tabia nzuri pamoja na kwamba mtendaji anaelewa kabisa ubaya wa tabia hiyo, yeye anaona ni tabia nzuri na pengine anajisifu kwamba yeye hawezekaniki na anaweza akafanya chochote atakacho.
Ikumbukwe kwamba maisha yetu yana taratibu zake za kuishi, hatuna uwezo wa kufanya vile tutakavyo.
Tunachojifunza hapa ni kwamba jambo lolote unalolirudiarudia (labda liwe zuri) kimsingi, siyo sifa, na ni tabia mbaya. Kuomba omba, kukopakopa, kuazima azima na kufanya fanya makosa sio ustaarabu mzuri kabisa na sio BUSARA katika maisha yetu ya kila siku. Kila kitu kina mipaka yake, tujifunze kuridhika na hali tulizo nazo kwa ajili ya maisha yenye furaha na amani.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania