Samaki Mmoja Akioza, Wote Wameoza?

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Nina imani wasomaji wengi wamewahi kusikia msemo huu kwani unatumika sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Bila shaka wengi wetu tumejikuta tunatoa maamuzi mabaya ama hukumu mbaya isiyokuwa na faida kutokana na kasoro ndogo zilizojitokeza mahali fulani.

Ninachowaeleza hapa ni mfano hai ambao ulinikuta wakati namaliza mafunzo yangu ya Kilimo ngazi ya Cheti. Alitokea kijana mmoja ambaye alikuja kujiunga pale Chuoni kama Mkufunzi (Agricultural Tutor) akitokea Chuo Kikuu Makerere. Yeye alikuwa mzaliwa wa mkoa wa Arusha. Huyo kijana alitokea kunipenda sana, wakati huo nimemaliza mafunzo yangu na nikabaki pale Chuoni kama kituo changu cha kazi.

Kijana huyo aliniganda sana. Alikuwa akimtuma hata Rafiki yake anieleze yaliyo moyoni mwake kuhusu mimi. Wakati ule ningali kijana nilikuwa nikijua kuwa mtu yeyote anayetoka Arusha ni Mmasai. Niliamua kuwa muwazi kwa rafiki yake nikamwomba amwambie kuwa mimi nawaogopa sana Wamasai kutokana na ninayosikia kuhusu wao kwamba:

  1. Wamasai ni wakali sana kwa wanawake.
  2. Wamasai wanatembea uchi.
  3. Wamasai ni watu ambao hawana dini
  4. Wamasai wanakula nyama mbichi.

Orodha yangu haikuishia hapo. Niliendelea kumwambia kuwa maisha ya namna hiyo sijayazoea hata kidogo na wala sitayaweza. Lakini pia itakuwa vigumu sana kuwaeleza wazazi wangu kuhusu huyu jamaa anayetoka kwenye kabila la ajabu ajabu. Nilimalizia kwa kusema kuwa kwa hakika, wazazi wangu hawataelewa kabisa.

Rafiki yake alifikisha ujumbe huu kama alivyoagizwa, naamini alitumia hekima na busara nyingi ili kukwepa kumuumiza kijana huyo. Maelezo ya rafiki yake hayakumtosheleza kijana huyo, hivyo Yeye na rafiki yake walikuja kwangu na akaanza kujitetea kwa kusema, “Mimi siyo Mmasai, mimi ni Mmeru, natoka Wilaya ya Arumeru.”

Kwa bahati mbaya maelezo yake hayakuniingia akilini kabisa. Kwangu mimi nilimuona kuwa huyu kijana ni mmoja wa hilo hilo kundi nisilolipenda. Niliona ni hao hao tu. Sikutaka kabisa kujihusisha nao.

Kwa bahati nzuri kwangu nilipata uhamisho kwenda Uyole Mbeya. Hili likabaki kuwa fimbo ya mbali haiui nyoka. Niliona kuwa nimejikomboa kutokana na hili, hivyo maisha yangu yalibakia vile niliyokuwa ninataka, kutokuwa na mtu mwenye asili ya Kimasai. Kwa dhati nilijiambia, yeyote na aje kwangu lakini siyo wa kabila la Kimasai.

Kutokana na simulizi hii, tunajifunza yafuatayo:

  1. Kamwe tusitoe hukumu ya jumla, iwe kwa mtu ama kabila. Ikumbukwe kuwa kila binadamu yuko tofauti na mwingine.
  2. Si busara kuona ubaya wa mtu mmoja kuwa ni ubaya wa familia nzima au ubaya wa kabila fulani ukawa ubaya wa kabila zins. Msemo wa samaki moja akioza, wote wameoza siyo sahihi kabisa kuutumia kwa binadamu, ingawaje mara nyingi tumeweza kufanya hivyo. Ni makosa, tena makosa makubwa. Kila mtu yapaswa ahukumiwe kivyake na si vinginevyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: