Nguo Ya Kuazima Haisitiri Makalio

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kwa kawaida nguo huvaliwa na mwanadamu ili kusitiri utupu wake. Hilo ndilo dhumuni la kwanza kabisa. Lakini kuna mitindo imezuka siku hizi ya watu kuvaa kwa ajili ya mashindano zaidi kuliko kusitiri miili yao. Utakuta lengo la mtu kuvaa ni kutaka aonekane kapendeza zaidi kuliko wengine. Pengine utakuta mtu anataka kuvaa kitambaa cha gharama kubwa sana ili mradi tu aonekane anazo, ni tajiri zaidi ya wengine.

Vivyo hivyo mtu anaweza akashona nguo yake mshono wa kutumia kitambaa kikubwa sana na kuifanya nguo itambae karibu barabara nzima, mithili ya nguo za mabibi harusi, ambayo hiyo huchukuliwa kama kawaida kwa nguo za hivyo, nguo za harusi. Wengi wetu ama sote tunazo nguo za kusitiri maumbile yetu. Kinachowaponza ni kutaka kuonekana tofauti na wengine na jamii inayowazunguka.

Wengine hudiriki hata kuazima magari kwa watu na hata kudiriki kutamani kuomba kukaa kwa muda kwenye majumba mazuri na ya gharama ili kuwaonyesha wakwe watarajiwa kuwa wako madaraja ya juu.

Haijalishi kama baadaye vitu hivyo vya kuazima itakupasa mwisho wake uje uvirudishe kwa wenyewe. Usemi busara hapo juu wa “Nguo ya kuazima haisitiri maumbile” ni fundisho tosha na kubwa kwetu sote, hususani wale wenye tabia ya kutoridhika na hali walizo nazo. Wakati mwingine mtu mwenye tabia hiyo mbaya huweza kuja kuaibishwa pale watu watakapogundua kuwa alikuwa anadanganta umma kwa kujifanya yeye ni matawi ya juu na kumbe hamna lolote. Sana sana mtu huyo ataishia kupata aibu kubwa na matusi kibao kwa ajili ya kujikweza kiasi hicho cha aibu wakati hana lolote.

Yatupasa wale wenye tamaa hizi tuache kabisa. Kila mmoja atakuchoka pamoja na watu wa karibu yako, ndugu na majirani. Kuazima kunaruhusiwa pale tu ambapo ni LAZIMA, mathalani kukiwa na msiba ama shughuli yeyote kubwa ya kijamii. Kuazima kwa kutaka sifa hakufai kabisa. Ridhika na kile ulichojaliwa ndugu yangu. Na pale utakapoazima, hakikisha unarudisha mara baada ya kutumia, na pia kiwe katika hali nzuri.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: