Kulala Maskini, Kuamka Tajiri

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Hakuna binadamu asiyependa kutiwa moyo katika maisha yake ya kila siku. Tumeumbwa na tunaishi duniani kwa viwango tofauti tofauti iwe kwa kipato, malazi, mavazi ama lishe. Kuna viwango vingine huweza kukatisha tamaa ya kuishi hapa duniani. Unaweza ukaona familia zingine zinaishi kwa tabu sana. Lakini tunakumbushwa kuwa hiyo isiwe sababu ya kukukatisha tamaa ya maisha maana hujui kesho yako itakuwaje. Huu ni msemo wa busara ambao umedhihirishwa wazi na mchezo wa Big Brother NAIJA uliomalizika muda mfupi uliopita huko Nigeria.

Mchezo huu ulihusisha vijana 32 wakike na wakiume na wa rika tofauti. Waliwekwa ndani kwa muda wa siku 72 bila kutoka nje. Humo ndani walikuwa wanapewa majukumu mbalimbali ya kufanya. Watu mbali mbali wa barani Afrika walikuwa wanaangalia mwenendo mzima wa hao vijana wakiwa humo ndani. Kila wiki watu zamani wa bara la Afrika walikuwa wanapiga kura nani wa atoke humo ndani, sababu kubwa ikiwa ni kutoendana na matakwa ya huo mchezo. Uchujaji uliendelea kufanywa mpaka wakabaki vijana 6. Ulipita muda, ikawa ndiyo siku ya kumpata mshindi wa BBA NAIJA.

Watu wa bara la Afrika walipga kura, akapatikana binti ambaye alikuwa ametokea kwenye familia moja ambayo ni duni sana tena sana. Alipotajwa binti huyu kuwa ni mshindi, alijitupa chini na kuanza kulia kwa furaha. Alisema kwa sauti kubwa sana “Asante Mungu”. Mshindi huyu alizawadiwa gari la Naira milioni 50, vyombo vya ndani na vingine vingi toka kwa wafadhili.

Kisa hiki kina mengi ya kutufunza, baadhi ya yale ambayo ni ya msingi sana ni:

  1. Katika safari yetu ya maisha hapa duniani hamna kukata tamaa
  2. Yatupasa tuishi maisha ya kujituma, kuwa waaminifu na kuwa watiifu pale panapobidi kufanya hivyo.
  3. Tutambue kuwa mapito mengi hapa duniani ni daraja yako ya kuvukia ng’ambo ya pili.
  4. Kumbuka kuwa unayopitia leo siyo utakayopitia kesho, mambo yanaweza kubadilika kwa sekunde tu na yakawa tofauti na unavyofikiri. Mungu wetu yuko kazini kila siku.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: