Aliye Juu Mngoje Chini

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Binadamu wote, maskani yao ni hapa chini. Hakuna mwanadamu yeyote ambaye makao yake yako juu. Kama mtu atabahatika kupanda juu, basi huwa ni kwa muda tu. Hatima yake ni chini, lazima atateremka tu.

Msemo huu una mafundisho makubwa sana. Tunafundishwa kwamba tupatapo fursa ya kuwa juu, hii inaweza kuwa kwa cheo kazini, au kwa kupata mali ama neema yoyote iwayo, tusijivune na kuwadharau wale walioko chini yetu. Ni lazima tukumbuke kuwa maisha ya mwanadamu ni ya kupanda na kushuka. Ni vema tukajua kwamba iko siku tutakuja kuwa chini na wale tuliokuwa tunawadharau wakaja wakawa juu.

Hali kadhalika, ni onyo kwa wale walioko chini, ambao hawana cheo ama mali na neema, wasije wakajisikia kuwa ni wanyonge mbele za hao walio juu ambao wanajivuna, maana siku yoyote na wao wanaweza wakashuka.

Hali kadhalika, msemo huu huweza kufananishwa na ule usemao, “mpanda ngazi hushuka”. Misemo yote miwili hutumika kumzindua mtu aliyepata cheo ama utajiri na hasa kama ameanza kujivuna kwa nafasi aliyopata, anaonywa asivimbe kichwa bure. Kama ambavyo hapo awali alikuwa chini, na sasa yuko juu, vile vile inawezekana sana siku moja akaja kushuka na kujikuta yuko chini. Maisha ndivyo yalivyo, hayana fomula maalumu. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: