Kichwa Cha Kuku Hakistahimili Kilemba

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Kuku ana kichwa kidogo sana ambacho kinalingana na ukubwa wa mwili wake ulio mdogo. Tunavyojua sote, kilemba ama kitambaa cha kichwa ni kikubwa sana ambacho kamwe huwezi kufikiria kumvalisha kuku kichwani. Endapo utajifanya mjuaji, ukamchukua kuku na ukamfunga kilemba, ieleweke kuwa hataweza kukibeba kwa sababu kitakuwa kizito sana kwake.

Msemo huu unaweza kutumika kwa mtu mwenye kichwa kidogo ambaye akipata cheo au nafasi hata ndogo tu, huanza kujivuna na kuwaona watu wengine si kitu mbele zake. Hujiona kuwa yeye peke yake ndiye bwana mkubwa sana na wengine wote ni vikaragosi mbele zake. Tunaweza kusema kuwa mtu huyu kichwa chake hakitofautiani na kichwa cha kuku ambacho hakiwezi kustahimili kubeba uzito wa kilemba. Kwa ulinganisho huu basi, mtu huyu hana uwezo wa kubeba cheo alichopewa.

Wako wengi tu ambao vichwa vyao ni vidogo na pengine hawastahili kubeba vyeo vikubwa ambavyo vinazidi uwezo wao.

Lakini endapo inatokea fursa kwa mtu kupata cheo kikubwa itampasa kichwa chake kidogo ‘akikuze’ kiwe kikubwa kiweze kustahili kuvaa ama kubeba kilemba ili kutimiza majukumu aliyopewa.

Kilemba chako kiwe ni dhamana, siyo cha kunyanyasia watu wengine na kuwaona ni takataka mbele zako.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: