Majukumu Ya Wazazi Kwa Watoto

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi …

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Nakumbuka nilipokuwa nasoma shule ya msingi nikiwa darasa la nne (shule hii iliishia darasa la nne tu), kulikuwa na mashindano ya michezo mbalimbali na katika mashindano haya shule yetu ilishika nafasi ya kwanza katika kila mchezo isipokuwa mbio za mita 200. Hata kwenye mchezo huu tungeweza pia kuwa wa kwanza ila ilitokea kuwa mtoto mwenzetu aliyekuwa katika ushindani tena akiwa wa kwanza bahati mbaya kaptula yake ilidondoka wakati akiwa karibu kabisa na kushinda mbio hizo kwa kushika namba moja.

Ilimbidi mtoto huyu asimame na kuikota suruali magotini ili aishikilie kiunoni na kukimbia kuelekea nyumbani kwao moja kwa moja. Shangilia yetu ilizimika, wenye kucheka walicheka na wenye kusikitika walisikitika, hususani wanafunzi wa shule yetu.

Mbaya zaidi, mtoto huyu kwa wiki nzima hakuja shule akiogopa kuchekwa na kutaniwa na wanafunzi wenzake. Hata hivyo hata alipokuja waliendelea kumcheka na kumtania, hivyo alikosa raha sana.

Adha hii ilitokea miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani wa kuingia darasa la tano. Mawazo mengi yalikuwa yanamsonga moyoni. Alionekana kabisa kukosa raha pale shuleni. Alikuwa anaumia ndani kwa ndani. Hivyo mtihani ulipowadia hakuweza kufanya vizuri. Alikuwa na msongo wa mawazo uliotokana na aibu aliyoipata mbele ya walimu na umati wa wanafunzi wenzake. Hakuweza kupata ushauri kutoka kwa mtu yeyote hivyo alikuwa nalo moyoni tatizo hilo lililomletea aibu.

Kisa hiki kina mafundisho kwa wazazi na walezi wa watoto. Yatupasa kuhakikisha unadhifu wa watoto wetu wawapo nyumbani na nje pia, mfano, shuleni ama mahali pengine popote. Endapo mzazi angelikuwa ameyaangalia mavazi ya mtoto wake kabla ya kwenda shule, angeliweza kugundua kuwa kaptura ilikuwa na dosari na hivyo angaliweza kuishughulikia mapema kabla haijamletea aibu mtoto wake mbele ya umami wa watu.

Yatupasa wazazi kuwa makini katika kuwaandalia watoto wetu nguo ama sare za shule, na hata baada ya kuvaa, yatubidi kuangalia kama nguo zimewakaa vizuri. Yaonekana kuwa kushindwa mtihani kwa mtoto huyu kulisababishwa na wazazi kwa kutokuwa waangalifu / makini na muonekano wa mtoto wao mbele za watu. Wazazi tunahimizwa kutekeleza vema majukumu yetu ya msingi kwa watoto wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: