Tusipende Kuhukumu Watu

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi …

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Alikuwepo mtu mmoja wa makamo aliyeishi katika kijiji kimoja kidogo. Mzee huyu alikuwa anachora na kuchonga sanamu nzuri na kuziuza sokoni kwa bei nzuri.

Siku moja, mtu moja aliyekuwa maskini alimshambulia mzee huyu kwa maneno kwa kusema, “Unatengeneza pesa nyingi sana kutokana na mauzo ya kazi zako za sanaa, lakini ni kwa nini huwezi kuwasaidia maskini hapa kijijini?”

“Je, humuoni huyu muuza nyama kuwa pamoja na kwamba si tajiri kama wewe, bado anagawa nyama za bure kwa maskini hapa kijijini? Pia hebu muangalie na huyo muoka mikate. Ni maskini na ana familia kubwa, lakini pamoja na hayo anatoa mikate ya bure kwa maskini hapa kijijini.”

Msanii huyu hakujibu lolote kwa shutuma alizotupiwa, bali alitabasamu tu na kuondoka.

Yule maskini alichanganyikiwa sana kwa kutojibiwa lolote na yule msanii, hivyo aliondoka huku akitangaza uvumi kwa watu kuwa msanii alikuwa ni tajiri sana lakini alikuwa mchoyo, aliyependa kujilimbikizia mali na hivyo hakuwa tayari kuwasaidia maskini.

Wana kijiji walimchukia sana huyo msanii na walifanya kila kitu ili kumtenga.

Baadaye yule mzee msanii aliugua na hakuweza kufanya chochote peke yake bila usaidizi kwani hakuna mwana kijiji hata mmoja aliyekuja kumtembelea. Hivyo hatimaye alikufa katika hali ya upweke mkubwa.

Siku zilipita, baadaye wana kijiji wakagundua kitu, kiliwashabgaza, muuza nyama aliacha kuwapa nyama bure maskini, na muoka mikate naye pia alisimama kutoa mikate ya bure kwa maskini.

Walipoulizwa muuza nyama na muoka mikate kulikoni, kwa nini hawaendelei kutoa misaada kwa maskini, walijibu: “mzee msanii ndiye aliyekuwa anatoa fedha kila mwezi kulipia nyama na mikate ya kuwapa maskini. Kwa vile sasa amekufa, hakukuwa na mtu mwingine tena wa kulipia chakula hicho cha bure. “

Kiukweli, watu wengi hapa duniani huenda wana maoni hasi na mitizamo tofauti juu yako. Cha msingi, usimruhusu yeyote kukubadilisha na kukuharibia jinsi ulivyo. Usipitishe hukumu juu ya mtu yeyote kutokana na muonekano wake ama kutokana na yale yanayosemwa dhidi yake.

Kuna mambo kuhusu maisha yake binafsi ambayo wewe huyajui.
Kama ungebahatika kuyajua ni mambo gani hayo ya kiundani wake, hakika, hukumu yako ingekuwa tofauti kabisa.

Mtu alikufa kwenye klabu ya pombe ama kwenye ukumbi wa muziki.
Mtu mwingine alikufa kanisani ama msikitini. Kama tungeweza kuwahukumu, tungeweza kusema kuwa mtu wa kwanza alikufa akiwa mdhambi na mtu wa pili alikufa akiwa mwenye haki, mtakatifu.

Lakini pengine mtu wa kwanza aliingia kwenye klabu ya pombe kwa lengo la kuwahubiria watu neno ili wasitende dhambi na yule wa pili aliingia kanisani kwa lengo la kuiba.

Kwa sababu hii, wewe na mimi hatuwezi tukaamua nani atakwenda Mbinguni ama nani atakwenda Motoni. Tumuogope Mungu sirini kwetu na tumuogope Mungu hadharani, mahali palipo wazi.

Muonekano wa mwanadamu huweza usitoe picha ya ukweli, picha ya uhalisia wake. Kwa hiyo samehe watu na sahau /dharau mapungufu yao. Tuombeane, tuwe wema kwa kila mtu, Tusikate mahusiano na binadamu wenzetu, eti kwa vile tu hawatufurahishi.

Dumisha umoja na mshikamano na kila mtu. Mungu aliyetuumba sote, anajua kila kilichofichwa mioyoni mwetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: