Ukiwa Na Tatizo Shirikisha Watu Wa Karibu Unaowaamini, Usikae Kimya

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi …

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika mkoa fulani palikuwa na wapenzi wawili, hatimaye walifunga pingu za maisha. Mume alikuwa anafanya kazi kiwanja cha ndege akiwa afisa mkubwa. Mkewe alikuwa muuguzi katika hospitali iliyoko mkoani humo.

Maisha yalienda vizuri wakafanikiwa kimaisha na pia wakapata watoto wawili. Zaidi ya hapo, mume alipandishwa cheo, nafasi ambayo ilimruhusu kuwa anasafiri nchi za nje mara kwa mara. Baada ya kuona watoto wao wadogo wanapata shida na wasaidizi wa kazi wa ndani, mume alimshauri mkewe aache kazi, mke naye aliafiki bila matatizo.

Kadri siku zilivyoenda mume wake alianza kubadilika tabia, akawa msaliti kwa mkewe na hata kusahau kuitunza familia yake. Ikawa hata ni shida sana kwake kuonekana nyumbani. Mke alimuomba sana Mungu ili tabia hiyo mbaya ya mume wake ibadilike, lakini badala yake hali ikawa mbaya zaidi na ikaendelea kuwa hivyo siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi na miaka baada ya miaka.

Mwisho mke wake alichoshwa na tabia hiyo. Akawa hana raha wala amani moyoni. Sonona ikamvaa barabara. Akakosa mahali pa kutulia mizigo iliyokuwa inamzonga moyoni mwake. Akawaza mambo mengi bila kupata majibu. Hali ikazidi kuwa mbaya sana hata akafikia maamuzi mabaya. Akili ilimtuma awaue watoto wake wote wawili pamoja na yeye mwenyewe pia. Alitimiza azma hiyo, na huo ndio ukawa mwisho wa uhai wa mama na watoto wake wawili. Inauma sana.

Tunajifunza mengi kutoka mkasa huu.

  1. Katika maisha binadamu tunapitia shida nyingi sana, ndogo na kubwa kupindukia. Uwezo wa kubeba matatizo / shida unatofautiana, mtu na mtu. Cha msingi usijione kuwa ni wewe peke yako unayepitia magumu, pengine wako wanaobeba mizigo mikubwa kuliko uliyoibeba wewe, hivyo usife moyo, usichukue maamuzi mabaya;
  2. Unapopata shida/tatizo, shirikisha mtu unayemuamini, usibebe uzito wote peke yako. Kwa kushirikisha wengine unaweza ukapata faraja na hasa pale utakapoambiwa kuwa wako wengi ambao wana matatizo makubwa pengine kuzidi yako na wanaendelea kuishi.
  3. Majirani/rafiki tujifunze kutambua shida zinazowapata wenzetu kwenye jamii zetu. Tuwe tayari kuwasaidia wasifikie hatua mbaya ya kuua na, ama kujiua. Endapo machungu yaliyokuwa yanamuumiza huyu mama yangeweza kugundulika ama kutambuliwa mapema na majirani, ndugu, jamaa ama marafiki na wakapata fursa ya kuongea naye na kumpa ushauri, pengine asingeweza kufikia hatua hiyo mbaya ya kutoa uhai wake na uhai wa watoto wake wawili.

Tunaweza KUZUIA vifo vitokanavyo na kujiua ama kuua. “TUJENGE MATUMAINI KWA VITENDO.” Kujiua/kuua HAKUKUBALIKI.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: