Tuwaheshimu, Tuwalee na Kuwatunza Wazazi Wetu Hata Kama Wamezeeka

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi …

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Jioni moja kijana mmoja wa miaka 28 aliamua kumpeleka baba yake katika nyumba ya kutunza wazee ili akaishi huko akisubiria siku zake za kuishi hapa duniani ziishe. Wazo hilo hakuliamua peke yake bali waliamua pamoja na mke wake kipenzi.

Hivyo, kulipokucha alimpeleka baba yake katika kanisa moja la karibu lililokuwa maarufu sana kwa kutunza wazee na watoto yatima.
Kiongozi wa kanisa hilo alikuwa Mchungaji mmoja, naye pia akiwa mzee sana. Alipomuona baba yake yule kijana, Mchungaji alimkimbilia na wakawa na mazungumzo ya muda mrefu sana.

Kijana alipoona wazee wamezungumza kwa muda mrefu vile ikabidi amuulize Mchungaji, “Samahani Mchungaji, kwani mnafahamiana na mzee wangu? Naona mmeongea kwa muda mrefu sana kama vile mnafahamiana vile tangu siku nyingi”.
Mchungaji akamjibu, “Ndiyo, namfahamu. Nakumbuka kati ya miaka 25 na 30 iliyopita, baba yako alikuja hapa na kumuasili (adopt) mtoto mmoja yatima tuliyekuwa tunamtumza ambaye alikuwa ni mgonjwa sana. Mtoto huyo alikataliwa na kila mtu lakini baba yako alikubali kwa moyo mmoja kumuasili. Isitoshe, huyu baba alikubali kuyabadili maisha ya yule mtoto kwa kwenda kuishi naye nyumbani kwake kama mtoto wake wa kumzaa. Hali kadhalika, alijitoa kwa hali na mali kumwendeleza yule mtoto kielimu na hata kimaisha.”

Mwishowe Mchungaji kwa uchungu mkubwa alisema, “Yule mtoto aliyekuwa mgonjwa sana na akaasiliwa na huyu mzee ni wewe.”

Kijana aliposikia hayo karibu adondoke chini kwa aibu. Alimpigia magoti baba yake akamwomba msamaha. Baba yake alicheka na kumwambia, “Tayari nimeshakusamehe mwanangu, mimi sikulaumu sana kwani huenda nilishindwa kukupa maadili ya thamani ya maisha (moral values of life). Umeamua kunitupa kwenye nyumba ya kutunzia wazee, nyumba niliyokutoa wewe kwa sababu mke wako anataka hivyo. Cha kushangaza, wewe hukufikiria kuongea na mimi kwanza. Basi na mimi nimeamua nikuachie nyumba yangu uishi mwanangu, lakini nimetengua wosia wangu niliokuwa nimekuandikia wewe kama mrithi pekee wa mali zangu zote. Hivyo basi, wosia wangu nimehamishia kwa hili kanisa ambalo watakuwa wakinitunza hadi siku nitakayoondoka hapa duniani”.

Kuna mambo muhimu ya kujifunza kwenye simulizi hii:

  1. Wazazi wetu ndio chanzo cha mafanikio yetu katika maisha yetu hapa duniani.
    Tusiwadharau wazazi
    hata siku moja
  2. Yatupasa kutambua kuwa wazazi wetu wametulea na
    kututunza kwa hali yoyote ile waliyokuwa nayo, hivyo wakizeeka ni zamu yetu kuwalea na kuwatunza na kuendelea kuwa na heshima kwao.
  3. Roho mbaya hailipi, mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: