Sikiliza Wosia Wa Waliokuzidi Umri

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi …

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Palikuwa na binti mmoja ambaye alijiona amechelewa kuolewa. Katika mtaa huo huo kulikuwa na kijana ambaye alikuwa kiwembe na mdanganyifu kweli kweli kwa mabinti. Kijana huyo alitokea kumchumbia yule binti. Wazazi wa binti walijaribu kumkataza asikubali kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na yule kijana.

Kwa bahati mbaya binti hakuelewa kabisa na hata alithubutu kumdharau mama yake. Kwa ujumla hakutaka kuchukua ushauri wa mtu yeyote, na hata marafiki zake aliwaona wanamghasi tu kwa kumwambia asimkubali mchumba ambaye atakuwa mume mtarajiwa.

Baada ya jitihada za kumkataza mahusiano na huyo kijana, wazazi waliamua kumuacha akae na maamuzi yake hivyo walimfanyia sherehe ya kumuaga ‘send off’ kubwa na ya uhakika kabisa.

Binti alifunga ndoa. Mungu aliwajalia kupata mtoto mmoja na huo ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo na mume wake. Shida zilianza, akawa hampi chakula na wala kutoa matunzo ya mtoto. Tabu zilipomzidi binti akawa anakwenda kula kwa mama yake mzazi ambaye alikuwa amemdharau sana hapo awali. Hali iliendelea kuwa mbaya zaidi, yakamshinda, ikabidi arudi nyumbani kwa wazazi wake.

Tuna mengi ya kujifunza kutoka hadithi hii.

  1. Yatupasa kusikiliza ushauri tunaopewa na watu, hususan, wazazi, ndugu na marafiki wanaotupenda. Maamuzi ya kuingia kwenye ndoa ni maamuzi makubwa na mazito sana, hayafanywi kimzaha mzaha ama kiholela holela tu. Tujiepushe na majuto yanayokuja baada ya kutenda bila kufikiri kwani majuto ni mjukuu.
  2. Tusiwadharua wazazi wetu kwani wazazi daima huwatakia mema watoto wao.
  3. Yaliyompata binti huyu yanaweza pia yakakupata wewe kijana. Vijana jihadharini na jitahidini kuwasikiliza wakubwa wenu kwani ‘Utu Uzima Dawa’. Wanapowaambia na kuwapa ushauri wa kimaisha mjue kuwa kuna mantiki ndani yake na mkisikiliza mtapata faida maishani

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: