Majina Yana Maana Hasi Ama Chanya?

Simulizi …

by GraceMshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Ni jambo la kubariki sana na la kuifurahisha jamii pale unapojitambua na kufanya mambo chanya.

Kuna mtoto mmoja aliyekuwa wa kipekee sana. Mtoto huyu alizaliwa kati ya watoto watano, alikuwa mtoto mwenye heshima kuliko nduguze wote. Mtoto huyu aliitwa Yabesi. Jina hili lina maana ya mtoto aliyezaliwa kwa huzuni. Hata hivyo haijulikani mama yake alikuwa na huzuni gani wakati anamzaa Yabesi, lakini ndilo jina alilopewa.

Yabesi aliendelea kukua na jina hilo lakini lilimpa shida sana. Aliogopa kuwa atakuwa mtu mwenye huzuni katika maisha yake. Ni kama vile taratibu za makabila ama watu wengine ambayo huwapa watoto wao majina ya Shida, Sikujua, Taabu, Sikudhani nk. Yabesi hakuishia kusikitika tu na kukaa kimya bali alimuomba mhusika mkuu amuondolee huzuni na kumbariki ili aweze kuwa mwenye furaha moyoni mwake na mbele ya jamii yake inayomzunguka.

Alianza kuwa na furaha moyoni, akabarikiwa sana kuliko ndugu zake. Familia na jamii wengine wakafanya nyumbani kwa Yabesi kama mahali pa kukimbilia wakiwa na shida zao. Walikuwa wakiomba ushauri mbalimbali kutokana na busara alizokuwa nazo Yabesi. Hali kadhalika alikuwa ni tajiri. Alikuwa ni wa msaada mkubwa sana kwa ndugu, jamaa na marafiki. Alikuwa ni mwema.

Kuna mambo ya kujifunza kwenye hadithi hii ya Yabesi.

  1. Vijana wajitambue na kuyatambua mazingira yanayowazunguka. Yale yaliyo ndani ya uwezo wao wajitahidi kuyadhibiti bila kukata tamaa.
  2. Tukiwa na mashaka katika maisha yetu tujue kuwa kuna mahali pa kukimbilia. Yatupasa tuyaache yale yanayoweza kudidimiza maendeleo yetu kwa kuishi tukilalama tu bila ufumbuzi.
  3. Wazazi tuwe waangalifu tunapotoa majina kwa watoto wetu. Mara nyingi jina unalompa mtoto wako huwa linaashiria vile atakavyokuwa. Mathalani kama ni jina la Shida mtoto anaweza kuishi kwa Shida. Jina la Furaha linaweza kuashiria furaha katika maisha ya mhusika. Kwetu sisi wazazi kama ni huzuni taabu ni sisi tumepata tusiwarithishe watoto wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: